Na Mathias Canal, Singida

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amezindua Mradi wa utambuzi na usajili wakazi waishio Wilayani humo wenye umri wa miaka 18 na zaidi ili kuhakikisha taarifa zao zinatambulika kitaifa na kimataifa ambapo Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA ndio wasimamizi wa zoezi hilo.

Akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo, Watendaji Kata, Waratibu elimu Kata, na Maafisa Kilimo wa ngazi ya Tarafa, Dc Mtaturu amesema kuwa Mradi huo utasaidia serikali kutambua wakazi wake wenye umri wa kuanzia umri wa miaka 18 ili kuainisha namna bora ya kuwawezesha vijana kupitia vikundi sambamba na umri wa zaidi ya miaka hiyo.

Mtaturu pia amewataka watendaji kusimamia vyema mapato ya serikali na kutoa risiti kwa kila malipo yanayofanyika ili ili kuepusha usumbufu kwa wananchi ambao wana jitahidi kwenda na kasi ya serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli lakini wanakwamishwa na baadhi ya watendaji.

Hata hivyo aliwataka watendaji hao kumaliza haraka matatizo ya wananchi ambayo yamekomaa na hatimaye kuwa sugu kwani  wasipofanya hivyo ni kukwepa majukumu yao hivyo kukosa siafa ya kuwa watumishi wa serikali kwani bado wana mtazamo hasi kwa kufanya kazi kwa mazoea.

Majukumu mahususi ya NIDA ni kutoa vitambulisho kwa Watanzania na wageni wakazi wa Tanzania na kutunza daftari la Utambuzi kwa lengo la kuimarisha usalama na amani, Kiuchumi na kijamii kwa maendeleo ya Taifa.

Dc Mtaturu alisema Mradi huo unatarajia hadi kufikia Disemba 31, 2016 usajili uwe umekamilika nchi nzima na kutoa namba ya utambulisho (NIN) kwa waombaji wote wenye sifa za kupewa kitambulisho vya Uraia.

Msimamizi Mkuu wa Mradi huo Agnes Mtei amesema kuwa miongoni mwa matarijo ya mradi huo ni pamoja na kuanza rasmi kwa matumizi ya vitambulisho vya Taifa katika upatikanaji wa huduma mbalimbali, kuboreshwa kwa huduma za jamii hususani upatikanaji wa huduma kwa haraka hasa zile zinazohitaji utambulisho na uhakiki, Upatikanaji wa taarifa kwa haraka na kupunguza ukiritimba katika upatikanaji wa huduma, Kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato (Kodi) pamoja na kuongeza idadi ya walipa kodi na Kuunganika kwa mifumo mbalimbaliya serikali na binafsi na hivyo kuongeza matumizi ya huduma kwa mfumo wa kielektroniki.

Mtei alisema kuwa katika kukamilisha zoezi hilo ni lazima kwa kila mwananchi, mgeni na mkimbizi anayeishi kihalali kujaza fomu ya maombi ya Vitambulisho ambapo kwa wale ambao hawana uwezo wa kujaza fomu hizo kwa sababu mbalimbali wanaruhusiwa kujaza/kujaziwa fomu hizo lakini lazima wathibitishe kuwa taarifa zilizojazwa ni za kwake na sahihi.

Mfumo wa usajili na utambuzi wa watu ni mfumo unaotambulika kwa chachu ya kukua kwa haraka kwa maendeleo ya kiuchumi duniani ambapo unatambulika kama mfumo wa kipekee katika mapambano dhidi ya vitendo vya kigaidi na mfumo utakao saidia kusukuma mbele mabadiliko ya haraka katika maendeleo ya nchi na mtu mmoja mmoja hivyo kutokana na jambo hilo serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikaamua kuanzisha mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA Agosti 01 Mwaka 2008.


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Mradi wa utambuzi na usajili wakazi waishio Wilayani hum
Wakuu wa Idara na Vitengo, Watendaji Kata, Waratibu elimu Kata, na Maafisa kilimo ngazi ya Tarafa wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa utambuzi na usajili wakazi waishio Wilayani humo
Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Bw Dandala Mzunguor akiwatambulisho waratibu kutoka Nida kwa ajili ya kutoa elimu ya namna ya kuendesha zoezi la utambuzi na usajili kwa wakazi


Kaimu Mkurugezni wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi Haika Massawe akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...