DC Daniel Chongolo-Longido
MKUU wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo amemwagiza Mkuu wa Polisi kumkamata na kumfungulia mashtaka Mhasibu Mkuu (DT) wa Halmashauri ya wilaya hiyo mkoani Arusha Issa Mbilu, kwa tuhuma za kuhusika na upotevu wa sh. milioni 84.

Akizungumza juu ya agizo hilo la kukamatwa Mhasibu huyo, Chongolo alisema uamuzi huo unatokana na upotevu wa fedha hizo zilizorudishwa na benki zilizokuwa zilipwe kwa watumishi hewa na wale waliokuwa na matatizo kazini.

"Leo (jana) tulikaa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ili pamoja na mambo mengine kukamilisha mchakato wa kupitia na kung'amua maendeleo ya kushughulikia tatizo la watumishi hewa. DT tulimwita ili asaidie kutoa maelezo katika eneo hilo.

"Tulipomhoji kuhusu fedha hizo zilizorudishwa na benki na kupaswa kurudishwa Hazina hakuwa na jibu. Nimeagiza polisi na vyombo vingine kufanya uchunguzi ili hatua za kisheria zichukuliwe juu yake,"alisema.

Alisema tayari polisi wanamshikilia Mbilu kutokana na tuhuma hizo na kwamba huenda wiki ijayo akapandishwa kizimbani kujibu tuhuma hizo.

Mkuu wa Wilaya Chongolo aliwaasa watumishi wote wa halmashauri hiyo kuwa makini na fedha za umma kwa kuwa hakuna atakaeonewa haya endapo atabainika kusababisha upotevu au kula fedha za umma.

Alisema yeye ndiye mwenye dhamana ya kusimamia uwajibikaji na nidhamu kwa watumishi wote wa serikali wilayani humo hivyo anataka kila mmoja kuona akitekeleza majukumu yake kikamilifu."Hatutakuwa na simile. Kila mmoja awajibike kwa kuzingatia sheria, utaratibu na maadili ya kazi. Tutakayembaini anakwenda kinyume na hapo tutamuwajibisha,"alisema.

Alisema anataka kuona Longido ikiwa ni miongoni mwa wilaya zinazokimbiliwa na wawekezaji kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya ufugaji kwa kuwa kuna rasilimali nyingi zenye uwezo wa kuinua uchumi wa Arusha na taifa kwa ujumla.

"Endapo kila mtumishi atatekeleza majukumu yake ipasavyo ni wazi wawekezaji watahamasika kuja kuwekeza katika wilaya yetu lakini hawawezi kufanya hivyo kama kutakuwa na matukio ya ajabu ikiwemo utafunaji fedha na urasimu,"alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...