Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani
Shinyanga, Stephen Magoiga amekutana na watendaji wa kata na vijiji
wilayani humo.
Magoiga amewataka hao kuhakikisha wanawajibika katika ukusanyaji wa
mapato ya Serikali badala ya kuacha watu wanakwepa kutimiza wajibu
wao.
Alisema watendaji wanapaswa kuhakikisha sheria za nchi zinafuatwa
ikiwemo kulipa kodi na ushuru mbalimbali ili Serikali ipate mapato na
kuweza kuwahudumia wananchi.
“Ukusanyaji mapato uwe ajenda muhimu na mtendaji ana uwezo wa
kulisimamisha gari lenye mzigo wa mazazo mahali popote kwenye himaya
yake na kuhakikisha limelipa kodi.
“Hakikisheni mageti yanafanya kazi ninyi ni walinzi wa amani katika kata
zenu kwa hiyo sitaki kuona sheria zinakiukwa, tuache kufanya kazi kwa
mazoea,” alisema.
Aidha, mkurugenzi huyo alionya tabia ya baadhi ya watendaji na
watalaamu mbalimbali kushinda maofisini badala ya kuwatembelea na
kuwahudumia wananchi.
Alisisitiza maofisini ni mahali pa vikao vya ndani tu na kuwa hatapenda
kuona wananchi wakikosa huduma kutokana na kutofikiwa na watalaamu
au watendaji.
Magoiga alitaka ushirikiano katika utendaji huku akikemea utoro katika
vituo vya kazi na kwamba mtendaji anapaswa kuhakikisha watumishi wote
ngazi ya kata wanakuwepo vituoni kwao.
“Utakuta mtumishi hayupo huku mtendaji kata hana taarifa yoyote hiyo ni
kazi ya mazoea, kila siku nasema sitaki kazi za mazoea, tuwajibike kwa
wananchi wetu,” alisisitiza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen
Magoiga (wa pili kushoto) akizungumza na watendaji wa kata na vijiji katika
kikao kazi kilichofanyika ukumbi wa halmashauri. Wengine pichani ni
kuanzia kushoto ni Afisa Utumishi na Utawala, Jumanne Chaula,
Mwanasheria wa Wilaya, Wilson Nyamunda na Afisa Kilimo, Umwagiliaji na
Ushirika Wilaya, George Kessy.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza na
watendaji katika kikao hicho.
Watendaji wa kata na vijiji wa Kishapu wakifuatilia maelekezo kutoka kwa
Mkurugenzi Mtendaji, Stephen Magoiga wakati wa kikao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...