Shule 450 zimefaidika na mradi wa INTERNET FOR SCHOOLS IFS kutoka kampuni ya simu ya Halotel.Shule hizo zimefungiwa vifaa maalumu vya kuwezesha upatikanaji wa intanet ya kasi shuleni kwa miaka mitatu bure bila gharama yoyote ili kuwasaidia wanafunzi kupata elimu zaidi, na kwenda na wakati katika kujifunza. Mradi huu ulianza mwaka 2015 na una makusudio ya kuzifikia chule nyingi kwa kadri iwezekanavyo. 

Katika kuwajali waalimu nchini kampuni ya Halotel pia imeanzisha huduma ijulikanayo kama CLOSER USER GROUP au CUG ambayo inawapa waalimu wote wanaotumia mtandao wa Halotel nafasi ya kujiunga na group na kuwasiliana kati ya wao kwa wao bure kabisa bila malipo kwa dakina 15 kila siku. Zaidi ya hayo, kila wakati mwalimu anapoongeza salio kwenye simu yake ya Halotel anapata bando ya GB1! 

Halotel haikuishia hapo katika kuboresha elimu Tanzania. Kampuni hiyo iliungana na Waziri mkuu mstaafu mh. Mizengo Pinda na kusaidia kujenga shule ya msingi ya kisasa kabisa Wilayani Mpanda mkoani Katavi. Halotel ilijenga chumba cha mikutano, chumba cha majadiliano, chumba cha kompyuta, pamoja na vyoo. Vyumba vyote hivyo pia havikuachwa vitupu bali viliwekwekewa samani, viyoyozi, na kila kitu ili kumboreshea mwanafunzi elimu.
Halotel pia imewasaidia wanafunzi wa shule tatu za Msingi mkoani Ruvuma kwa kuwapa Mabegi ya kisasa kwa ajili ya ubebaji na utunzaji wa vitabu na madaftari yao.
Kampuni ya Halotel pia imetoa madawati katika shule zilizoko mkoani Tabora, Kagera, pamoja na Geita.Pamoja na kusaidia kuchangia katika sekta ya elimu, kampuni ya Halotel inaahidi kuwapa watumiaji wa mtandao wao huduma bora za simu na intanet zilizo juu kuliko zozote zile Tanzania!
"Diwani wa Chalinze na Mfanyakazi wa Halotel wakimsikiliza mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Luboga ambayo imepata nafasi ya kupewa chumba cha compyuta na intaneti katika mradi wa Halotel kuboresha elimu."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mimi natumia internet yao halotel, kiukweli wapo vizuri. Hata kwenye voice, embu jaribu siku moja kuongea na sim ya halotel ukiwa kwenye lift sim haikatiki lakini ukiutmia mitandao mingine huwa inakata au hamsikilizani. Hiyo mimi nilishangaa.

    ReplyDelete
  2. hivi wanatumia wireless au wired network mpaka kufikia kwenye computer za hizo shule

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...