Na Mdau wa Anga 
Shirika letu la ndege lilikufa kwa sababu ya kushindwa kujiendesha kutokana na gharama kubwa za uendeshaji pamoja na ufinyu wa abiria 
wanaotumia usafiri wa anga! Mwanzo nilifikiri labda ni wizi unafanyika lakini baada ya kujua gharama chache za uendeshaji nikaona ni sawa kwa shirika hili kushindwa kujiendesha. 
 Naomba nianze na bei ya Boeing Boeing ambayo inauzwa dola milioni mia mbili tisini na sita (US296millions) wakati Bombardier Q400 inauzwa dola milioni 35 tu (US35millions) Kumbe badala ya kununua Boeing moja ni heri tuongezee dola milioni kumi na tisa (US19millions) tununue Bombardier tisa (Bombardier 9) Hesabu yake Boeing price=US296Millions Bombardier Price=US35Millions (35×9=315) 315-296=19  Ambapo hizi Bombardier tisa zingetusaidia kwa upande wa shirika kujiendesha lenyewe na kutupatia faida kubwa kwa mara tisa kwa Taifa. 
 Kuhusu speed ya Boeing ni kweli ni kubwa kuliko Bombardier kutokana na uchomaji wa mafuta...Speed yake ni 590mph wakati speed ya Bombardier ni 414mph au 667km/h Kama kutoka Dar to Mwanza ni Km 1100 maana yake Bombardier itatumia lisaa limoja na dakika arobaini (1 hr and 40mnts) wakati Boeing itatumia lisaa limoja na dakika kumi na tano(1hr and 15 mnts) tofauti ni dakika 25 tu.
               Boeing inatumia dumu moja la mafuta la lita 4 kwa sekunde moja kwa hiyo kwa lisaa limoja inatumia lita elfu kumi na nne mia nne (14,400) (4l×60s×60m) 
 Kwa mfano Mafuta ya ndege kwa lita yakiuzwa shilingi 2000 maana yake ili tutie mafuta ya kuelekea safari ya Songea inayochukua takriban lisaa limoja tu tunahitaji milioni 28,800,000(14,400×2000) Na tunahitaji abiria 96 watakaolipa Tsh 300,000 ili kuweza kulipia gharama za mafuta tu 
 Hapo hatujajumlisha gharama za service na wafanyakazi na wala hatujapata faida yoyote Bombardier inatumia 1.187lita ya madumu ya mafuta kwa mile moja yaani ukikadiria inatumia lita moja ya mafuta kwa mile moja  (1mile=1.6kms) Songea to Dar Air Distance ni takribani kilometa 537=335.625miles Kwahiyo itatumia lita 398.386875 ambazo ukizizidisha kwa gharama ya Tsh 2000 kwa lita unapata laki saba tisini na sita elfu mia saba sabini na tatu=796,773 Kiuchumi kugharamika 28,800,000 na kugharamika 797,000 bora kipi? 
 Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu na mwenye kutaka shirika hili kujiendesha kwa kibiashara ni lazima atumie Bombardier ili apate faida. 
 Pia kutokana na hali ya viwanja vyetu ndege hizi zinasuite kwasababu zinaweza kutua katika viwanja vya kawaida ndio maana serikali ilizinunua ndege hizi mahususi kwa safari za ndani! 
Hizi ndege Bombardier Q400 zinatumika Marekani na wanaendelea kununua.  Shirika la ndege la American Eagle wanazo Bombardier 35 Uingereza nao shirika la ndege la Flybe wamenunua 40. Australian Air wamenunua 20 Ethiopia wamenunua 4 kufikisha idadi ya Bombardier 19. 
Hatuwezi kutenga bajeti ya serikali iende ikahudumie shirika la ndege ambalo ukitumia akili ya kiuchumi hili shirika linaweza kujiendesha na likaliletea faida Taifa na kuliinua kiuchumi. 
Hatupo kwa ajili ya kujishow off kutumia ndege za gharama kubwa na zisizo na faida ili watu watuone tuna ndege kubwa no! 
Tupo kwa ajili ya kuliendeleza Taifa letu kwa faida liendelee mbele. Sijawahi kuona upinzani uliokosa hoja Duniani kama upinzani huu uliopo Tanzania Walianza na argument ya Twiga kwenye ndege ati Twiga kachorwa vibaya mguu, wamefika kwenye ndege ati Pangaboi na sasa hivi wamekosa cha kusema wanaongea kuhusu Water Canon Salutation. Wameona hawana mashiko sasa hivi wanabeza seats,Shame upon you! 
 Watanzania kwa pamoja tuliendeleze Taifa letu,tujali maslahi ya Taifa kwanza kuliko kitu chochote! Hawa wapuuzi wachache wanaobeza juhudi za Mh Rais Dr John Pombe Magufuli kuliendeleza Taifa letu tuwapuuze na kuwadharau! Tuwasikilize watu wenye mapenzi mema na Tanzania!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...