Sallam kutoka WCB ameonyesha baadhi ya nyaraka ambazo zimewapitia kibali cha kutumia sehumu za wimbo ‘Maria Salome’ wa Saida Karoli katika wimbo mpya wa Diamond, ‘Salome’.
saida-karoli

Wimbo ‘Maria Salole’ wa Saidi Karoli ni miongoni mwa nyimbo za asili zilizofanya vizuri miaka ya 2000.Hali hiyo iliufanya uongozi wa Diamond kuzungumza na uongozi wa Saida Karoli ili upate kibali cha kutumia sehemu za nyimbo hiyo.
“Tunakushukuru sana uongozi wa Saida Karoli na mzee Felician Mutakyawa kutupa haki na baraka zote kutumia wimbo wa Maria Salome,” aliandika Sallam instagram. “Tunatambua kwamba nyimbo hii itaendelea kuwa moja ya nyimbo bora kuwahi kutoka katika nchi ya Tanzania,”
Diamond kupitia wimbo huu amerudi tena katika nyimbo za asili baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Mdogo Mdogo’ miaka miwili iliyopita.
Pichani juu anaonekana Diamond na Rayvanny wakiwa na Mzee Felician Mutakyawa wakati wa kusaini makubaliano ya kutumia sehemu ya wimbo huo wa 'SALOME' ambao umebamba kila kona.
CHANZO: BONGO FIVE


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hakuna mwengine zaidi ya Diamond.

    ReplyDelete
  2. Aisee Naseeb, hapa ndipo anapowaacha mbali artists wengine wa Bongo kwa ubunifu wake.... Diamond hakika yupo juu, wengine watafuata nyuma tuu, watake wasitake.
    Endelea na uzi huo huo!

    ReplyDelete
  3. jamaa anajua sana

    ReplyDelete
  4. Masha Allah! Kwa kweli hii 'version' ya 'Maria Salome' iliyoimbwa na Diamond Platnumz ft Rayvanny, ipo very 'classic'. Hakika mnastahili pongezi za pekee kwa kazi nzuri, kuanzia midundo (muziki) , uchezaji na hata ujumbe 'makhsusi' uliyomo katika wimbo huo, kwa kweli wenye wivu wajinyonge tu. Hakika mnastahili sifa na pongezi za pekee 'crew' nzima ya WCB kwa ushirikiano wenu.

    ReplyDelete
  5. Safi sana,, ila kama haujasoma magazeti ya leo basi SOMA HAPA

    ReplyDelete
  6. Sanaa ni ubunifu, mmeutendea haki huu wimbo, mmewaacha 'kodo', hongereni sana Diamond na team nzima ya WCB

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...