Na Mwandishi wetu

Mrembo, msanii wa filamu na mwanamuziki, Jokate  Mwegelo ametoa wito kwa jamii, mashirika na watu binfasi kujitolea kusaidia wahanga wa tetemeko la Ardhi lililoikumba  mkoa wa Kagera na kusababisha vifo na baadhi ya watu kukosa makazi ya kuishi.

Jokate  alitoa wito huo jana wakati wa kutangaza mikakati yake ya kusaidia wahanga wa tetemeko hilo kwa kushirikiana na Taasisi ya GSM Foundation. Alisema kuwa tikio hilo ni kubwa na lemeleta majonzi kwa baadhi ya familia na kuwaomba wadau kuungana kusaidia kuondoa changamoto zinazowakumba wahanga.

Alisema kuwa wakati anajipanga chini ya msaada wa GSM Foundation, ameamua kutoa rai kwa watanzania ikiwa pamoja na wanamichezo, wasanii, wanamuziki na wadau wengine mbalimbali kuchangia ili kuondoa changamoto  hizo.

“Kwa kweli hali si nzuri kabisa, mimi kama msanii na ni Mtanzania, nimeguswa na kuamua kuingia mtaani kuhamasisha watu binafsi, makampuni  na asasi mbalimbali kuunga mkono juhudi za serikali kusaidia wahanga wa tetemeko hilo,” alisema Jokate.

Alisema kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kuungana katika tatizo hilo ambalo pia limeharibu baadhi ya shule na kusababisha wanafunzi kukosa sehemu ya kupata elimu. “Kwa wasanii, warembo na wanamuziki, ni wakati muafaka sasa kusaidia  na kufanya mrejesho wa mapato yetu kwa jamii kwa kusaidia wahanga,” alisema.

Alifafanua kuwa suala hili si kwa watu wenye uwezo,tu, bali hata watu wenye kipato kidogo  linawahusu kwani chochote walichonacho kama nguo, vyombo vya nyumbani, vitanda, magodoro, chakula, sabuni, mafuta na vitu vingine vinahitajika kwa wahanga wa tetemeko hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...