Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006, mbunifu wa mavazi na mwanamuziki , Jokate Mwegelo kwa kushirikiana na kampuni ya GSM Foundation amesaidia waathirika  wa tetemeko la ardhi wa mkoa wa Kagera kwa kukabidhi magodoro 400.
Jokate ambaye pia ni msanii wa luninga alikabidhi magodoro hayo kwa mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja  Jenerali mstaafu, Salum Kijuu makoa makuu ya mkoa huo.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Jokate alisema kuwa  kampuni ya GSM Foundation nay eye wameguswa na athari za tetemeke hilo ambalo mbali ya baadhi ya watu kupoteza maisha, kuna waathirikia mbalimbali.
Jokate alisema kuwa kuna watu wamepoteza makazi yao ya kuishi na mali zao mbalimbali, jambo ambalo limewafanya kurudi nyuma katika kimaisha.
Alisema kuwa magodoro ni moja ya mahitaji makubwa ya wahanga katika mkoa huo kuamua kukabidhi kontaina la futi 40 kwa Mkuu wa Mkoa.
“Ni janga la kitaifa kwani waliokumbwa na matatizo hayo ni watanzania wenzetu na wanahitaji msaada mkubwa, kuna majeruhi, kuna waliopoteza wazazi na jamaa zao huku wanafunzi wakikosa sehemu ya kusomea,” alisema Jokate.
Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali  Mstaafu, Salum Kijuu aliwashukuru Jokate na kampuni ya GSM Foundation kwa msaada huo ambao utapunguza changamoto za wahanga wa  tetemeko hilo.
 “Namshukuru Jokate na kampuni ya GSM Foundation kwa msaada huu, ni msaada mkubwa, lakini bado tunahitaji misaada zaidi, bado kuna changamoto nyingi sana kwa wahanga, hivyo tunaomba mashirika, watu binafsi  na wadau wengine waunge mkono katika janga hili,” alisema Kijuu.
Alisema kuwa kama kila Mtanzania atachangia sh 100, wataweza kukusanya jumla ya Sh bilioni 5 ambazo zitawasaidia kuondoa changamoto mbalimbali na kuwafanya wahanga kurejea katika maisha yao ya kawaida.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu (kushoto) akizungumza mara mara baada ya kupokea moja ya magodoro 400 yalitolewa na Kampuni ya GSM Foundation kupitia kwa Miss Tanzania namba 2 wa mwaka 2006, Jokate Mwegelo (kulia).

 Jokate Mwegelo akizungumza mara baada ya kukabidhi magodoro hayo ambayo yametolewa na kampuni ya GSM Foundation kwa wahanga wa tetemeko la ardhi la mkoa wa Kagera.
 Jokate Mwegelo akizungumza na baadhi ya watoto yatima ambao nyumba yao waliyokuwa wanaishi iliathirika na tetemeko la ardhi. Jokate kwa kupitia kampuni ya GSM Foundation walisaidia watoto hao baadhi ya magodoro.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu (wa pili kulia) pamoja na Miss Tanzania namba 2 wa mwaka 2006, Jokate Mwegelo (kulia) mara baada ya kupokea magodoro 400 yalitotolewa na kampuni ya GSM Foundation.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...