Na Mwandishi Wetu
Wazazi nchini wametakiwa kuwa na moyo wa kujali afya za watoto wao hasa zinapotokea fursa za tiba za bure kwenye jamii zao kwani ni nadra sana kwa fursa hizi kujitokeza katika jamii za kitanzania. 

Hayo yamesemwa na mbunge wa Chalinze Mhehimiwa Ridhwani Kikwete alipotembelea kambi ya madaktari Bingwa wa Mifupa na mishipa ya fahamu kutoka taasisi ya MOI ambao wako katika kambi tiba ya GSM Foundation, inayozunguka nchi nzima kuwafanyia upasuaji watoto waliozaliwana vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa nusu Kaputi, Bw. Ogutu Ogonga mara baada ya kutembelea kambi ya madaktari Bingwa wa Mifupa na mishipa ya fahamu kutoka taasisi ya MOI ambao wako katika kambi tiba ya GSM Foundation, inayozunguka nchi nzima kuwafanyia upasuaji watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi mapema leo Mjini Kibaha - Pwani. 

Huu ni mkoa wa 10 kwa kambi hii kutembelea, huku ukiwa ni msimu wa tatu wa kambi tiba hizi zenye lento la kuokoa miasma ya watoto takriban 3500 wanaohisiwa kupoteza maisha kila mwaka köa mujibu wa tafiti za MOI za mwaka 2002, ambazo zinasema zaidi ya watoto 4000 huzaliwa kila mwaka lakeni ni 500 tu huweza kufika kwenye tiba huku changamoto kubwa ikitajwa kuwa ni uchache wa madaktarim ba ukubwa wa gharama za tiba. 

Awamu ya kwanza ya kambi tiba ya GSM ilipita mikoa ya Mwanza, Shinyanga. Singida, Dodoma na Morogoro. Ya pili ikapita Mtwara, Songea, Mbeya na iringa. Hii awamu ya tatu itapita katika mikoa ya Pwani, Tanga, Kilimanjaro na Mara.
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiongea na Kaimu Mganga Mkuu hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani - Tumbi, Dk Aggey Geoffey(Wa pili kutoka kushoto), na Dk Silas Msangi( Wa kwanza kushoto), mara baada ya kutembelea kambi ya madaktari Bingwa wa Mifupa na mishipa ya fahamu kutoka taasisi ya MOI ambao wako katika kambi tiba ya GSM Foundation, inayozunguka nchi nzima kuwafanyia upasuaji watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi mapema leo Mjini Kibaha. Kulia ni Afisa uhusiano wa GSM Foundation Khalphan Kiwamba. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...