KAMPUNI ya KFC Kuku Foods Limited Tanzania wametoa msaada wa 
vifaa vya braille kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kuona na kusikia wa shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko iliyopo kariakoo jijini Dar es Salaam.

Katika halfa ya makabidhiano ya vifaa maalum kwa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko iliopo Kariakoo, KFC Meneja Mkuu wa KFC Tanzania, Louis Venter
amesema kuwa vifaa hivyo vitawasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum ambao ni wasio na uwezo wa kuona na wale wasioweza kusikia Vile vile Msaada huo ni muundelezo wa ushirikiano na uhusiano wa karibu kati ya Kampuni ya KFC na Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko. 

Meneja Mkuu wa KFC Tanzania Bwana Louis Venter amesema, “ Dhumuni la Mchango wetu ni kusaidia kuboresha mazingira ya kijamii ya watoto hawa. Tunataka mchango huu wa kampuni yetu uwe wa maandalizi ya uzinduzi wa programu maalum iitwayo ‘Add Hope Program’ ya kusaidia jamii nchini Tanzania mwezi Oktoba mwaka huu.”

Kampuni ya KFC imedhamiria kutoa msaada kwa shule hii yenye mahitaji maalum kwa kipindi endelevu.
Meneja Mkuu wa KFC Tanzania, Louis Venter akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko pamoja na wafanyakazi pamoja na walezi wa wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma katika shule hiyo jijini Dar es Salaam na kutoa msaada wa vifaa vinavyowasaidia watoto wenye ulemavu wa macho(Upofu).
Baadhi ya wafanyakazi wa KFC watitoa msaada wa vifaa vya braille kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kuona na kusikia kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mshana jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...