Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo  Mhe. Nape Moses Nnauye ameahidi kutoa shilingi laki tano kwa kila goli litakalofungwa na timu ya Serengeti Boys  katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 unapigwa jioni ya leo katika Uwanja wa Taifa dhidi ya Timu ya vijana ya Congo-Brazzaville.

Akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mhe. Nape amesema milango ipo wazi kwa wadau wengine wa michezo kujitolea katika kuiwezesha timu na hivyo kufanya vizuri katika  mechi hii ambayo ni muhimu sana kushinda ili kufuzu kwa fainali hizo.

“Hii timu ni yetu sote hivyo inahitajika tuimiliki, tuepe nguvu, tuiombee ili iweze kufanya vizuri na hatimaye kufuzu kuingia fainali kwa kuitoa timu ya Congo-Brazzaville” alisema Mhe. Nape.

Waziri Nape amekutana na wachezaji wa timu hiyo ili kuwapa maneno ya faraja kabla ya kuanza kwa mechi na kuwataka watanzania  kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuwapa motisha wachezaji kwa kuwashangilia  na kuwatia moyo.

Mbali na hayo Waziri Nape alitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya kadi za kieletroniki zilizozinduliwa hivi karibuni kwa kueleza kuwa kadi hizo bado hazijaanza kutumika rasmi ila zitaanza kutumiwa katika mchezo baina ya Wabunge wa Simba na Yanga pamoja na Bongo Fleva.

Timu ya Serengeti Boys inaundwa na vijana wa Kitanzania wenye umri chini ya miaka 17 ambapo katika mchezo huo watahitaji ushindi na baadaye kufanya mechi ya marudiano mnamo Oktoba 2 mwaka huu nchini Congo-Brazzaville.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo  Mhe. Nape Moses Nnauye akipena mkono na mmoja wa wachezaji wa timu ya Taifa ya Vijana "Serengeti Boys" alipokutana nao mapema leo asubuhi. Kushoto ni Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...