Siku kama ya  19 September ndio siku ya kuzaliwa mkuu wa bendi ya Ngoma Africa aka FFU  Ughaibuni ya kule ujerumani, Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja (pichani) aliyezaliwa mjini Dar-es-Salaam, akiwa mtoto wa kwanza wa kiume wa Bw.Jumanne Saleh Makunja Ngayonga (RIP) na Bi.Moza Hassan Seif Mpili (Mama Makunja), Mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja leo ndio Happy Birthday  yake !!!!!


Kamanda huyu wa FFU Ughaibuni amepewa zawadi ya mlinzi mwingine mbwa aina ya Bulldog mwenye  umri wa mwaka moja na nusu amepewa mafunzo maalumu na ana uwezo wa kukimbia mita 300 kwa sekunde 4. Na akikung'ata ni sawa na kudondokewa na chuma kilo 40 pia ana nguvu ya kasi ya kuangusha kwakupiga kikumbo kilo 75. Mkuu huyo wa Ngoma Africa band apewa pia sanamu la mbwa kwa kuweka getini kwa kutaadharisha watu.
Unaweza kuburudika na kusherekea naye katika kambi yao FFU-Ughaibuni at http://www.ngoma-africa.com auwww.ngoma-africa.com
Ungana nao pia at www.facebook.com/ngomaafricaband

GLOBU YA JAMII INAUNGANA NA WAPENZI WA NGOMA AFRKIKA BAND HERI YA KUZALIWA KWA KAMANDA RAS MAKUNJA AMBAYE ANAPEPERUSHA VYEMA BENDERA YA TANZANIA UGHAIBUNI. TUNAMTAKIA MAISHA MEMA NA MAREFU YEYE NA DOGI SURA MBAYA MPYA ALIYEMPATA KAMA ZAWADI. HONGERA SANA KAMANDA!
- ANKAL

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...