Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa akisalimiana na
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali Salum Kijuu alipomtembela leo ofisini kwake kumpa pole kutokana na athari ya tetemeko la ardhi katika mkoa wake
Na Mwandishi Wetu-KAGERA.

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa ameipongeza Serikali kwa namna ilivyojipanga kukabiliana na athari za tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo.

Bw. Lowassa amesema hayo kupitia salamu zake alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali Salum Kijuu, ofisini kwake kumpa pole kutokana na athari zilizotokana na tetemeko hilo.

“Napenda nikupongenze mkuu wa mkoa kwa namna ulivyokabili tukio hili, wala hatukuwa na mashaka wewe ni mtaalam wa majeshi wa siku nyingi kwa hiyo jambo hili limempata mwenyewe mpiganaji na tunaona kwa pamoja mmelishikilia vizuri,” alisema Lowassa.

Adha Mhe. Lowassa alisema kuwa suala hili ni kubwa na halipaswi kuiachia Serikali peke yake katika kulikabili nalo kwani madhara yanaonekana ni makubwa hivyo watanzania wote wana budi kuwasaidia waathirika.

Katika kushirikiana na wananchi wa Kagera, Bw. Lowassa ameahidi kutoa mifuko 400 ya saruji kwa ajili ya ujenzi ya miundombinu iliyoharibika.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja, Generali Salum Kijuu ameendelea kuwasisitiza watanzania kuchangia kile walichonacho ili kusaidiana na serikali katika kuwafariji waathirika wa tetemeko hilo.

“Tunashukuru watanzania kwa misaada wanayoendelea kutoa kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko ila bado tunaendelea kuwasisitiza tuendele kujitoa kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye mahitaji,” alisema  Meja Generali Salum Kijuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. MKUU, LOWASSA KILA MARA NASIFU SANA SIASA ZAKO, TAZAMA MANENO ULIYOSEMA JUU YA TUKIO NZIMA, NA ULIVYO MWAMBIA MKUU WA MKOA, HIYO NDIYO SIASA TUNATAKA TANZANIA SIO VITA,TAZAMA UMEIPONGEZA SERIKALI KWA NJISI ILIVYOJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA TETEMEKO LA ARDHI, KIZURI UNAKISEMA KIBAYA UNAKISEMA,
    MUNGU AKUBARIKI SANA, SIASA SIO VITA, TANZANIA KWANZA.
    DR, JAMESSY.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...