Walimu wa Home Gym wakikata keki ya maadhimisho ya miaka 18 kwa pamoja katika sherehe zilizofanyika fukwe za Escape One mwishoni mwa wiki.
 Keki maalum
Wanachama wa Home Gym Wakiwa katika mazoezi mbalimbali

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MKURUGENZI wa Kituo cha kufanyia mazoezi ya viungo Home Gym, Andrew Mangomango amesema kuwa kwa mwaka huu maadhimisho ya miaka 18 toka kuanzishwa kwake yatazunguka katika baadhi ya mikoa.

Akizungumza wakati wa maadhimishi hayo yaliyifanyika Katika fukwe za Escape One mwishoni mwa wiki, Mangomango amesema kuwa ndani ya miaka 18 ameweza kupata wanachama wa kudumu takribani 200 na ameweza kuwasaidia watu mbalimbali kufahamu jinsi gani ya kufanya mazoezi.

Mangomango amesema kuwa, maadhimisho haya ni ya tano mfululizo na kwa mwaka wameamua kutembelea baadhi ya mikoa ikiwemo Tanga, Arusha na Mwanza ambapo baadhi ya wanachama wake wa siku nyingi wapo kule na watatumia fursa hiyo kuhamasisha watu mbalimbali kufanya mazoezi kwa afya.

"Na katika kuendeleza michezo, Kituo cha Home Gym kimeweza kutoa walimu takribani nane ambao wote wameshafungua Gym zao mikoa mbalimbali, hii ni moja ya mafanikio tuliyoyapata na zaidi bado tunashirikiana nao na hata leo kwenye maadhimisho haya wapo wote wamekuja kuunga mkono jitihada za Home Gym,"amesema Mangomango.

Katika maadhimisho yaliyohudhuriwa na baadhi ya wadau wa michezo ikiwemo Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG, Imani Kajura, waandishi wa habari mbalimbali na taasisi zingine wameonyesha muitikio mkubwa wa kufanya mazoezi na kuhamasisha watu wajitokeze kwani Michezo ni Afya.

Kwa mwaka huu, Mangomango amesema kuwa mwaka huu watafanya maadhimisho yao sambamba na Kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Oktoba 14, mkoani Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...