Waziri Mkuu Mhe.  Majaliwa Kassim Majaliwa akipokea Mfano wa hundi ya shilingi Milioni 16 kutoka kwa mratibu wa magrupu ya Whatsapp ya LEADERS NA UONGOZI, Dk. Ave Marie Semakafu katika hafla fupi ya makabidhiano hayo ambayo imefanyika ofisini kwa Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na mratibu wa magrupu ya Wasap, Dk.Ave Marie Semakafu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachanachama wa magrupu ya Whatsapp ya LEADERS  FORUM NA JUKWAA LA UONGOZI   katika hafla fupi ya makabidhiano hayo ambayo imefanyika ofisini kwa Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam leo.
----------------------------------------------------
Imedhihirika kuwa magrupu ya Whatsapp  yanaweza kuwa chachu ya Maendeleo  baada  ya wanachama wa magrupu mawili ya whatsapp ya LEADERS FORUM na  JUKWAA LA UONGOZI  leo Septemba 22, 2016 kumkabidhi Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa jumla ya shilingi  16m/-, kwa ajili kusaidia waathirika wa tetemeko  la ardhi mkoani Kagera.

Akizungumza katika hafla hiyo, mmoja wa waratibu wa magrupu hayo Dk.Ave Marie Semakafu amesema fedha hizo ni michango ya wanachama wa magrupu hayo yenye jumla ya wanachama 491. Amesema wanachama hao wameguswa na yaliyowakuta Watanzania wenzao mkoani Kagera hivyo waliona njia pekee ya kuungana nao katika majonzi ya janga hilo ni kutoa kidogo walichonacho. 
Dk Semakafu amewaasa watanzania wengine, hasa walioko kwenye vikundi mbalimbali hususani vya mitandaoni, kushiriki katika zoezi hilo la kuwachangia waathirika hao kwa vyovyote wawezavyo, maana hali bado ni mbaya mkoani Kagera. Hatua hiyo ni ya kwanza kwa magrupu ya mitandaoni nchini Tanzania kufanya harambee na kukusanya pesa kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la Ardhi mkoani Kagera.
Dkt Semakafu alisema madhumuni ya magrupu hayo ni kujadili maendeleo ya Taifa pamoja na kutoa ushauri mbinu mbadala kuifikia ndoto ya Tanzania tunayoiyaka.
Tetemeko hilo lilitokea Septemba 10, mwaka huu ambapo watu 17 wamepoteza maisha,wengine zaidi ya 200 wameruhiwa,huku nyumba zaidi ya 800 zikiwa zimeharibika,zingine kuanguka. 
Akiongea katika hafla hiyo Waziri Mkuu Majaliwa aliwashukuru wanachama wa majukwa hayo akisema wanapaswa kuwa mfano wa  kuigwa na makundi mengine nchini. 
 "Sisi kama serikali tunawashuru sana kwa moyo huo wa upendo kwa wenzetu wa Kagera,na hatutaishia hapa bali tutafanya hivyo kwa maandishi", alisema Waziri Mkuu na kuyaahakikishia wachangiaji waliokabidhi misaada yao leo yakiwemo  makampuni mbalimbali na vikundi vingine vitano kuwa atahakikisha misaada yote itawafikia walengwa.

Wanachama wa majukwaa hayo ni watu wa kada mbalimbali hususani viongozi wa serikali wa sasa na wastaafu,akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Mizengo Pinda.Wengine ni Mawaziri,Wabunge, wakuu wa mashirika ya umma na binafsi, wanataaluma wa vyuo vikuu, wanahabari, Wafanyabiashara na Viongozi wa vyama vya Siasa.

Waratibu wengine wa magrupu hayo ni Dereck Murusuli,Benjamin Thompson Kasenyenda,Leila Sheikh, Dr.Michael Francis, Maggid Mjengwa, Mustafa Ismail Kambona, Zamaradi Kawawa na June Warioba. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...