Jengo ambalo ndani yake kuna tanuri la kuchakata makaa ya mawe ambalo limejengwa kwa msaada wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ikiwa moja ya mkakati wake wa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuanzisha na kutumia nishati mbadala kunusuru Misitu nchini. Jengo hilo linatumiwa na Shirika Lisilo la Kiserikali la Mbalawala Women Organization (MWO).
NA HAMZA TEMBA - WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Misitu ni muhimu kwa maisha ya binadamu na viumbe hai kwakua huifadhi vyanzo vya
maji, kuboresha hali ya hewa, kuzuia mmomonyoko wa ardhi, upatikanaji wa kuni,
mbao, madawa, malisho ya mifugo, kuboresha shughuli za kilimo na kuboresha
mandhari ya nchi yetu mijini na vijijini.
Aidha, misitu pia ni chanzo muhimu
cha mapato kwa wananchi wengi wa vijijini na mijini.
Ni kutokana na
umuhimu huo wa Misitu ndio maana Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS)
akapewa jukumu la kusimamia misitu na rasilimali zake kwa niaba ya Serikali Kuu
ili iweze kuwanufaisha watanzania wa leo na wa vizazi vijavyo kupitia matumizi
endelevu.
Iko wazi kuwa kuna
utegemezi mkubwa wa misitu kama chanzo rahisi na kikuu cha nishati nchini,
ambapo zaidi ya asilimia 90 ya nishati inayotumika Nchini inatokana na miti.
Uvunaji mkubwa wa mkaa umeathiri sana ubora wa misitu. Kuni zinatumika zaidi
vijijini na mkaa unatumika zaidi mijini.
Moja ya mashine inayotumiwa na Shirika Lisilo la Kiserikali la Mbalawala Women Organization (MWO) kuchakata makaa ya mawe kwa ajiliya matumizi ya majumbani. |
Matumizi ya nishati mbadala
yanatajwa kama moja ya suluhisho la tatizo hilo, Katika kukabiliana na tatizo la
uharibifu wa Misitu Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za
Misitu nchini (TFS) inafanya ushirikiano na wadau wa sekta mbalimbali hasa Wizara ya Nishati na madini na jamii kwa
ujumla ili kupunguza utegemezi wa misitu kama chanzo kikuu cha nishati.
Miongoni mwa asasi za
kiraia ambazo Wizara inashirikiana nazo katika kuhamasisha matumizi ya nishati
mbadala ni Shirika Lisilo la Kiserikali (NGO) la Mbalawala Women Organization (MWO) ambalo lipo katika wilaya ya
Mbinga Mkoani Ruvuma, Makao yake makuu yakiwa katika kijiji cha Ruanda eneo maarufu
kwa jina la Center D.
Shirika hilo limejikita
katika uwezeshwaji wa vikundi vya wanawake kiujisiliamali ili waweze kujikwamua
kiuchumi hasa wanawake ambao wanazunguka mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka uliopo
Kata ya Ruanda wilayani Mbinga, wengi wao wameshindwa kuajiriwa na mgodi huo
kutokana na ugumu wa shughuli husika ambazo hufanywa na wanaume.
Likiwa limejikita na
shughuli za miradi ya utengenezaji wa vitofali vya kupikia vya makaa ya mawe pia
lina lengo la kutunza mazingira kwa kupunguza ukataji wa miti kwa kutengeneza
na kuhamasisha jamii juu ya matumizi ya nishati hiyo mbadala.
Akizungumza na Mwandishi wa Makala hii, Meneja wa Uzalishaji wa shirika hilo, Harid Kapinga aliitaja miradi mingine
ambayo inafanywa na shirika hilo kuwa ni huduma ya chakula na usafi katika
kambi ya mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka, programu ya shule, bustani ya mboga
na matunda, shamba la mpunga na ufinyanzi wa vyungu.
Akizungumzia uongezaji wa
thamani wa makaa ya mawe ili yaweze kutumika kwa matumizi ya majumbani, Meneja
huyo wa Uzalishaji alisema, awali wananchi walikuwa wanaokota makaa ya mawe
pembezoni na mgodi na kwenda kupikia bila kujua madhara yake kwa maisha ya
binadamu na uharibifu wa vyombo ambavyo walikuwa wanavitumia katika kupikia
vyakula vyao.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...