Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka wafanyakazi wa kiwanda cha kuchakata gesi asilia kilichopo Madimba mkoani Mtwara wawe wazalendo na wafanye kazi kwa bidii katika kulinda na kuutunza uwekezaji huo mkubwa ambao serikali inautegemea katika uzalishaji wa nishati ya umeme wakati taifa linaelekea kwenye nchi ya viwanda.


Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wafanyakazi na watendaji wa kiwanda hicho baada ya kutembelea kiwanda kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa kiwandani hapo akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Mtwara.


Amesema kiwanda cha kuchakata gesi asilia ni hazina kubwa  kwa Taifa hivyo ni kikalindwa na kutunzwa ipasavyo kutokana na umuhimu wake katika uzalishaji wa nishati ya umeme kwa maendeleo ya nchi.


Makamu wa Rais pia amewashukuru na kuwapongeza wafanyakazi wa kiwanda hicho cha kuchakata gesi asilia cha Madimba na amewahakikishia kuwa serikali itaendelea kuwajali na kuwathamini katika utendaji wao wa kazi na kwamba serikali itahakikisha wafanyakazi wa kiwanda hicho wanapewa motisha ya kutosha ili waongeze maradufu utendaji wao wa kazi ili malengo ya serikali ya kuleta maendeleo kwa wananchi kupitia viwanda inatimia kwa sababu taifa litakuwa na nishati ya umeme ya uhakika.


Makamu wa Rais amewataka watendaji wa Shirika la Maendeleo la Petroli (TPDC) ambalo linasimamia mradi huo kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kusaidia huduma za jamii katika vijiji vinavyozunguka mradi huo kila mwaka ili wananchi waweze kuwa walinzi wa mitambo hiyo.
Akitoa maelezo mafupi ya mradi huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. James Mdoe amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuchakata gesi ya futi za ujazo milioni 210 kwa siku.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akitembelea kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba Mhandisi.Leonce namna gesi inavyopokelewa na kuchakatwa na kusafirishwa kwa watumiaji
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiangalia mfumo wa uendeshaji na usalama wa kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Next time tafadhalini wahusika, inapotokea hafla mithli ya hiyo, kiongozi yeyote katika hiyo high table ya mikutano kama hapo pichani, basi at least mumuwekee japo 'Disposable Glass' kama hata 'Bilauri' itakosekana. Nimeona hapo pichani Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Hassan Suluhu. mmemtengea chupa ya maji basi hata gilasi au kikombe hakuna aliyekumbuka kumuwekea, mathalan angetaka kunywa hayo maji ndio aanze 'kupiga tarumbeta' na yeye au..?! Hayo tufanyiane sisi kwa sisi, lakini sio kwa viongozi wetu tena wa ngazi za juu, namna hiyo nakhisi kama inachusha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...