Gari la kubebea wagonjwa [Ambulance] lenye thamani ya mill.80 lakabidhiwa katika kwa mkurugenzi na mkuu wa wilaya wa Mufindi na MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa ametoa msaada wa gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa iliyopo katika jimbo lake hilo.

Mgimwa alikabidhi gari hilo ikiwa ni moja ya ahadi yake aliyoitoa wakati akiomba kura kwa wananchi wa jimbo la mufindi kaskazini katika kampeni ya uchaguzi mkuu 2015,ambapo alisema kutokana na changamoto ya uhaba wa gari ya kubebea wagonjwa katika zahanati na vituo vya afya katika jimbo hilo, endapo atapewa ya kuwa mbunge atahakikisaha gari ya wagonjwa linapatikanaili wagonjwa waweze kufika hospital kwa wakati.

Akizungumza na wananchi wakati wa kukabidhi gari hilo,mbunge Mgimwa alisema muda wa kupiga siasa umeshapita na kazi iliyopo hivi sasa ni kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuwatatulia changamoto zinazowakabili.Alisema pamoja na kuongeza gari ya wagonjwa atahakikisha anaboresha vituo vya Afya vilivyopo katika jimbo lake ili kupunguza wimbi kubwa la msongamano wa wagonjwa wanaokuja kutibiwa katika Hospitalini ya wilaya.

‘’’Nipo kwenye mchakato wa kuboresha vituo vyote vya Afya ndani ya jimbo langu,na nitahakikisha huduma muhimu zinapatikanaikiwa pamoja na dawa za kutosha na vifaa mbalimbali vinavyohitajika ili wananchi wangu waweze kuhudumiwa bila usumbufu katika vituo hivyo,hii itasaidia kupunguza msongamano katika hospitali ya wilaya’’’’’alisema Mgimwa

Aidha katika mkutano huo mbunge alisisitiza swala la uaminifu kwa watumishi waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi wahakikishe wanajikinga na vitendo vinavyoashiria rushwa ,vinavyoweza kuwaharibia sifa ya utendaji kazi zao na kushindwa kuwajibika ipasavyo katika majukumu yao.

‘’’Sisi wabunge,madiwani na mtumishi yeyote aliyepewa dhamana na wananchi anatakiwa ajiepushe na swala zima la rushwa ili aweze kutenda haki kwa kuwatatulia changamoto wananchi wake waliomchagua. Tunatakiwa tuwatumie wananchi kuwaletea maendeleo ipasavyo na si vinginevyo’’’alisema

Jamhuri William ni mkuu wa wilaya ya Mufindi,akipokea msaada wa gari hilo kutoka kwa mbunge Mgimwa alisema gari hilo litaweza kusaidia kuokoa vifo vya wanamufindi hasa mama na mtoto ambapo hapo awali kuliwa na gari moja tu.
MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi
MBUNGE wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi huku wananchi wakiwa kwa pembeni
na hii ndio sehemu ya ndani ya gari la kubebea wagonjwa alilokabizi mbunge wa Mufindi kaskazini,Mahamood Mgimwa akikabidhi gari hilo kwa viongozi wa wilaya ya mufindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...