Naibu Waziri wa TAMISEMI Sulemani Jafo akihutubia wadau wa kampeni ya kuchangia Madawati Mkoa wa Geita kwenye Harambee iliyofanyika Mjini Geita.
Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii katika Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Elias Kasitila akitoa maelezo kuhusu namna Acacia ilivyoshiriki mwaka huu kuchangia kwenye zoezi la madawati.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu Bwana Graham Crew akiwa amenyoosha mikono kusalimia umma wa Watanzania waliongana kwenye harambee ya madawati Geita.
Timu ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri baada ya Meneja wa Ustawi na Mahusiano ya Jamii katika Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Elias Kasitila kutanga kuwa Mgodi utatoa shilingi milioni Mia Moja kwa ajili ya madawati Mkoa wa Geita.

Na Dixon Busagaga.

Akitangaza kiwango hicho katika hafla ya changizo iliyofanyika Desire Park Mjini Geita , Meneja Ufanisi na Mahusiano na Jamii wa Mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu bwana Elias Kasitila amesema, “Bulyanhulu imebarikiwa kuwa karibu na Wilaya mbili,Halmashauri ya Msalala iliyopo Mkoa wa Shinyanga na Nyang’wale iliyopo Mkoa wa Geita. 

“ Hivyo basi tulipopokea mwaliko kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale kuhusu kampeni ya leo ya madawati tumeamua kwamba japokuwa miradi mingine ya madawati tumeifanya mkoa wa Shinyanga tumeona kuna umuhimu wa kufanya hivyo mkoa wa Geita pia.”alisema Kasitila. 

"Hivyo basi siku ya leo tunajitolea kuchangia Tsh100m/- kwa ajili ya kampeni za mikoa inayolenga kuondoa upungufu wa madawati 70,000.”aliongeza Kasitila. 

Elias aliongeza kuwa, “misaada ya madawati kutoka kwenye migodi iliyoko chini ya Acacia ambayo ni, North Mara, Buzwagi and Bulyanhulu,kwa mwaka huu Acacia imetumia takriban fedha za kitanzania zaidi ya Billion Moja ambayo inakadiliwa kutengeneza zaidi ya madawati 10,000. 

Mgeni rasmi katika hafla ya kuchangia madawati mkoa wa Geita alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa ambaye aliwakilishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi ,Utumishi na Utawala Bora, Mh.Suleiman Jafo. 

Akiwahutubia washika dau waliokuwa Desire park Naibu Waziri Jafo alisema “Nitapeleka salamu kwa waziri mkuu kuhusiana na mwitikio ambao nimeushuhudia leo ninaagiza kamati ya Kampeni ya madawati Geita kuorodhesha washika dau wote waliochangia leo na kuwasilisha orodha hiyo kwenye ofisi ya Waziri Mkuu ili binafsi awatambue wote walioonesha kuguswa kuiondolea Geita uhaba wa madawati.” 

Katika hafla hiyo Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Aacacia Bulyanhulu Graham Crew binafsi alijitolea kuchangia fedha za kitanzania shilingi 750,000/- kwa ajili ya kampeni hiyo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tumalize swala la madawati na madarasa tuanze kuangalia uboreshaji wa elimu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...