Rais wa Mchezo wa Wushu, Mwalami Mitete akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa mashindano ya Wushu yanayotarajiwa kuanza kesho kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Gola Kapipi na Kushoto ni Makamu wa Raisi Kawina Hadji Konde.
MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa michuano ya Wushu Tanzania inayoanza kesho Septemba 17 na 18 kwenye uwanja wa Taifa kuanzia saa 4 asubuhi.

Mchezo wa Wushu ambao asili yake ni nchini China unajumuisha Karate, Kung Fu, Judo na aina zote za michezo yote ya mapigano kitu ambacho kitakuwa ni kivutio kikubwa kwa watakaohudhuria.

Mashindano hayo yatahusisha washiriki mbali mbali toka mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani,Morogoro, Lindi, Mtwara, Pemba pamoja na Mbeya.

Rais wa chama cha Wushu Tanzania Mwalami Mitete amesema washindi wa mashindano hayo watapata medali, fedha taslimu, vikombe, Simu za mkononi pamoja na vyeti vya utambulisho ambavyo vitawawezesha kushiriki mashindano mbali mbali ndani na nje ya nchi.

Mitete amesema kuwa kumekuwa na dhana potofu kuwa michezo ya mapigano ndiyo chanzo cha machafuko lakini amekanusha vikali na kusema ni kama zilivyo fani nyingine na ajira pia kwakua inaweza kuwaingizia washiriki kipato.

Naye Balozi wa Utamaduni wa China nchini Gao Wei amesema wataendelea kushirikiana na chama hicho ili kuhakikisha mashindano hayo yanaendelea kufanyika kila mwaka yakiwa yameboreshwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...