Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka  nchini China , waliotaka kufahamu maeneo mbalimbali ya uwekezaji yaliyopo Mkoani Arusha,mzungumzo hayo yalifanyika ofisini kwake.
Amewahakikishia kuwapa ushirikiano,mazingiza mazuri  na usalama kwa wawekezaji kutoka China watakaofika kuwekeza katika Mkoa wa Arusha, na watakapoitaji msaada wowote kutoka Serikalini basi watapatiwa kwa wakati.“Kwa Mkoa wa Arusha mtapata ushirikiano wakutosha kutoka Serikali na mtakapoitaji msaada sehemu yoyote katika utendaji wenu wa kazi basi msisite kuwasiliana nasi na tutawasaidi”,alisema Gambo.                          Kutoka ubalozi wa China kwa Tanzani bwana Gou Huodong,amemwakikishia Muheshimiwa Mkuu wa Mkoa kuwa ataenda kuwahamasisha wachina wengine waliopo China kuja kuwekeza zaidi Mkoani Arusha hasa kwenye sekta ya Utalii ambayo ndio inayokuwa kwa kasi sana na inaongeza pato la taifa kwa asilimia kubwa.“Nitaenda  kuwahamasisha wenzangu huko China waje kwa wengi hapa Mkoani Arusha kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbalia hasa ya Utalii kwasababu sekta hii inakuwa kwa kasi sasa,”alisema Gou.Pia Muheshimiwa Gambo aliwaelezea mpango wakufunga Kamera za barabarani(CCTV) kwa Mkoa wa Arusha ilikuimalisha zaidi ulinzi na Usalama hasa kwa wawekezaji na watalii wanaoingia katika Mkoa huu, na hivyo kuwaomba waangalie hiyo fursa kwa upande wao iliwaisaidie Serikali katika kuimalisha ulinzi wake maeneo mbalimbali ya Mkoa.Ugeni huu kutoka ubalozi wa China hapa nchini ulikuwa na lengo kubwa lakuweza kufahamu maeneo mbalimbali ya uwekezaji yaliyopo katika Mkoa wa Arusha, kwakuwa wageni wengi kutoka China waliofika katika Mkoa wa Arusha walikutana na mazingira mazuri ya uwekezaji.
Mjumbe kutoka ubalozi wa China nchini Gou Huodong,akielelezea jinsi atakavyowahamasisha wawekezaji wengi kutoka China waje kuwekeza Mkoani Arusha,pembeni ni Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,akipeana mkono kama ishara ya ushirikiano baina ya nchi ya China na Mkoa wa Arusha na Mjumbe kutoka ubalozi wa China Nchini Gou Huodong.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe kutoka nchini China na Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...