Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

MKURUGENZI wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella ameziweka hadharani nyumba takribani tano za wasanii wake wa kundi la Yamoto Band na kuwataka wananchi waelewe kuwa msanii anahitaji nyumba na sio magari.

Nyumba hizo zilizojengwa nje ya mji kidogo, Katika kata ya Kisewe amesema kuwa hiyo ni moja ya maendeleo kwa wasanii ,kwani hii si mara ya kwanza kuwazawadia nyumba wasanii wake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Fella amesema kuwa ameamua kuziweka wazi hasa baada ya kusikia maneno mengi kutoka kwa wananchi wakidai kuwa Yamoto Band hawafaidiki na Muziki wanaoufanya.

Fella amesema kuwa nyumba hizo mpaka sasa hajajua thamani yake ila zitakapokamilika ataita watu wa tathmini kwa ajili ya kuziangalia ili kujua zimetumika kiasi gani kwenye ujenzi huo.

Ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa juhudi kubwa sana alizozifanya katika kuhakikisha anafanikiwa kuinua wasanii. Na katika nyumba hizo zitakazozinduliwa hivi karibuni zitapatiwa kwa Wasanii wanne wa Yamoto Band na Mshindi wa BSS 2015 Kayumba Juma.

Meneja wa Mkubwa na Wanawe, Amani Temba 'Mh. Temba' amesema kuwa hizi nyumba zimejengwa kwa fedha za wasanii wenyewe wanazozipata kwenye shoo za muziki wanazozifanya na sio kama hela zinazotoka mfukoni mwa kiongozi yoyote.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Twanga Pepeta Asha Baraka amefurahishwa na hatua hii kwani ni mara chache sana kwa viongozi wa muziki kuchukua dhamana ya kuwajengea nyumba vijana hawa wadogo na amewataka wasanii kutokufanya mzaha kwenye tasnia hii.

Fella amezindua pia nguo aina mbalimbali zenye nembo y Yamoto Band na wamezilipia Brela,COSOTA kwa hiyo yoyote atakayejaribu kunakili watamshughulikia.

Nyumba za Wasanii wa Yamoto Band zikionekana kwa muonekano wa nje.
Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella akikagua kwa ndani nyumba za wasanii hao zilizojengwa nje ya mji Eneo la Mbande Kisewe.

Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella akikagua kwa ndani nyumba za wasanii hao zilizojengwa nje ya mji Eneo la Mbande Kisewe.

Mkurugenzi wa Kituo cha Mkubwa na Wanawe Saidi Fella akikagua nyumba ambazo zipo kwenye hatua ya mwisho ya umaliziaji.
Mkurugenzi wa Kituo cha Mkubwa na Wanawe Saidi Fella akionyesha baadhi ya bidhaa zenye nembo ya Yamoto Band zitakazopatikana nchi nzima

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...