MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo amemuagiza mkurugenzi wa jiji la
Arusha, Athumani Kihamia kulipa madeni yote wanayodai walimu ya
milioni 154 ndani ya wiki mbili ambayo wamekuwa wakidai serikali
kuu kwa muda mrefu bila kulipwa na hivyo kusababisha walimu hao
kukata tamaa ya ufundishaji wanafunzi .

Gambo alitioa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na walimu wote wa
shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha ,waratibu elimu,wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata katika mkutano wa kujua changamoto zinazowakabili walimu hao ili zipatiwe ufumbuzi.

Alisema kuwa walimu wamekuwa wakifundisha katika mazingira magumu na kwamba hadi sasa wapo walimu wa shule za msingi wanaoadai madeni ya likizo na mengineyo yenye gharama ya milioni 154 ambapo serikali kuu
ndio inayopaswa izilipe na hadi sasa hawajalipwa jambo ambalo
linawafanya walimu hao kupoteza muda wa kufundisha na kufuatilia kila
siku madeni hayo.

“mkurugenzi nakupa muda wa wiki mbili deni hili la milioni 154 kwa
ajili ya walimu akikisha zinalipwa haraka iwezekanavyo wakishalipwa
ndio upambane na serikali kuu ufidie hapo zilikotolewa kwani
haiwezekani walimu wapoteze muda kila siku wakifuatilia tu madeni huku
wakiwa wameacha vipindi bila kufundisha wanafunzi wetu”alisema Gambo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji hilo,Athumani Kihamia akijibu agizo
hilo alilopewa na mkuu wa mkoa alisema kuwa fedha hizo ambazo ni
madeni hayo zinapaswa zitokee serikali kuu na kwamba atahakikisha
kuwa ndani ya muda wa wiki mbili atazilipa kupitia fedha za ndani za
halamshauri hiyo ili zikija zirejeshwe.

Alifafanua kuwa deni hilo atalipa kutoka kwenye fedha alizoziokoa
ambazo zilikuwa zinalipwa kinyume cha sheria kwa madiwani ambapo
kiasi cha milioni 130 zilizokuwa zinatumika kuwalipia madiwani
mafuta ,simu pamoja na nauli zitaelekezwa kulipa walimu hao madai
yao ili waweze kujikimu na hali wanayokabiliana nayo.

‘‘Fedha ambazo zimeokolewa kwa ajili ya mafuta ni milioni 40.8,fedha
za simu za madiwani milioni 61.2,nauli iliyookolewa milioni 28 ambapo
jumla ni milioni 130 ambazo zimelipwa kinyume hivyo fedha hizi
zinaelekezwa kwa walimu wa msingi na sekondari ikiwa ni madeni
wanayodai halmashuri hii ambapo fedha zinasubiriwa serikali kuu lkni
tumeona tuwatangulizie hizi fedha ili wajikimu na waweze kufundisha
watoto wetu vizuri”alisema Kihamia .

Kihamia alisema kuwa watatanguliza fedha hizo kwa walimu hao wakati
wakiwa wanasubiria fedha toka serikali kuu ili waendelee kujikimu
kwani zimeokolewa katika mianya ambayo zilikuwa zinateketea hivyo
zitaongeza ufanisi kwa walimu katika kufundisha wanafunzi na akili
zao na kufanya akili zao kuzielekeza kwa wanafunzi ili wapate elimu
bora.

Baadhi ya walimu hao wakieleza kero zao walisema kuwa wanakabiliwa na
tatizo la kutopandishwa madaraja kwa waliokaa kazini muda mrefu huku
wengine walioingia kazini muda mfupi wakiwa wanapandishwa madaraja
bila kujua vigezo hivvyo kumwomba mkuu wa mkoa kuingilia swala hilo.


MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo akiongea na walimu wote wa shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha ,waratibu elimu,wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata .
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro akiwa anaongea na walimu waliohuthuria mkutano huo.Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
.

wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa jiji la ArushaAthumani Kihamia akiwa anasikiliza kwa makini malalamiko ya walimu hao.
picha ya juu na chini ni walimu waliouthuria mkutano huo wa mkuu wa mkoa uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa AICC uliopo mkoani Arusha.
Habari picha na Woinde Shiza-Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...