Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe akiwaasa wakurugenzi, meya na wenyeviti wa halmashauri zote
saba Mkoani Singida  katika kikao cha Jumuiya za Serikali za mitaa Tanzania (ALAT).
Wakurugenzi, meya na wenyeviti wa halmashauri zote saba Mkoani Singida  wakiendela na katika kikao cha Jumuiya za
Serikali za mitaa Tanzania (ALAT).
……………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu Singida
 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amewaasa
wakurugenzi, meya na wenyeviti wa halmashauri zote saba Mkoani Singida kutumia vikao vya mafuzo ya Jumuiya za Serikali za mitaa (ALAT) kutatua kero za halmashauri.
 
Mhandisi Mtigumwe ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya ALAT
mkoa wa Singida na kuwasisitizia kuwa mafunzo hayo yawe na tija na sio kukaa vikao visivyo na matokeo chanya.
 
Ameongeza kuwa katika kipindi cha miezi sita tangu ateuliwe na
Mhe Rais amebaini halmashauri zina changamoto za ukusanyaji hafifu na
usioridhisha wa mapato ya ndani pamoja na mikataba mibovu inayosainiwa na halmashauri na hivyo kuiletea hasara serikali.
 
Mhandisi Mtigumwe amesema kumekuwa na migogoro ya ardhi
inayosababishwa na maafisa ardhi wasio kuwa waadilifu, watumishi na madiwani,kujimilikisha ardhi na vibanda kinyume na utaratibu pamoja na kutotengwa kwa asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa ajili ya wanawake na vijana.
 
“Halmashauri hazijatenga maeneo ya viwanda vidogo na vya kati,
uchafu umekithiri katika maeneo mengi, watumishi wanaokiuka taratibu
hawachukuliwi hatua za kinidhamu na mawasiliano hafifu kati ya viongozi na watumishi, viongozi na viongozi na hata watumishi wenyewe, hizi ni baadhi ya changamoto ambazo kikao cha ALAT kitumike kuzitafutia majibu, alisisitiza.
 
Mhandisi Mtigumwe amewasisitiza wakurugenzi kuunda mabaraza ya
wafanyakazi na halmashauri zenye mabaraza hayo basi vikao vifanyike ili kero na changamoto za watumishi zisikilizwe na kutafutiwa ufumbuzi.
Kwa upande wao meya, wenyeviti na wakurugenzi wa halmashauri
wamemshukuru mkuu wa Mkoa kwa nasaha alizowapa na kuahidi kuyatumia mafunzo ya ALAT katika kuleta mabadiliko katika halmashauri zao.
 

Wajumbe walipata fursa ya kujifunza juu ya Mfumo ya serikali za
mitaa Tanzania bara, ukusanyaji wa mapato ya ndani kwenye halmashauri,
utaratibu wa manunuzi katika serikali za mitaa , uwazi na uwajibikaji na
mawasiliano kwa viongozi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...