Mkuu wa wilaya Nachingwea Mhe. Rukia Muwango anawashukuru wale wote walioitikia wito na waliojitoa kwa hali na Mali kuchangia mkono wa pole kwa wenzetu wa Kagera waliopata maafa ya Tetemeko la ardhi, hata ambao hawakuweza kutoa chochote.
"Tunashukuru kwa maombi yao kwa kuwa tunajua walikuwa na nia njema, Tunatambua mchango wa kila mmoja kwa namna yapekee kabisa. 
"Kiasi kilichopatikana taslimu ni shilingi 5,576,000/-. Na nguo kiasi. Tutatoa taarifa ya mwisho siku ya Jumatano. Bado tunaendelea kupokea michango hadi tarehe 27, mwezi huu  saa 5 usiku. Tunashukuru kwa ushirikiano. 
"Ni imani yetu kuwa TUTAENDELEA NA MOYO HUU HASA KWA WITO WA KUCHANGIA MAENDELEO YETU WANA NACHINGWEA. Asanteni sana", alisema DC Muwango.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...