Anitha Jonas – WHUSM.
MUSWADA wa Huduma za Vyombo vya Habari  kusomwa kwa mara ya kwanza Bungeni  Septemba hii na  kujadiliwa  Desemba Mwaka huu.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye alipokuwa akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA kilichorushwa na  TBC 1,chenye lengo la Mawaziri kueleza umma namna wanavyotekeleza majukumu.

“Muswada huu mzuri na utasaida kuleta suluhishi la malalamiko ya kuwepo kwa sheria kandamizi,pia itasaidia kukuza tansia ya habari pamoja na kuifanya tasnia ya habari kuheshimiwa kama tansia nyingine”,alisema Waziri Nnauye.

Waziri Nnauye alisisitiza kuwa uandaaji wa Muswada  ulishirikisha wadau mbalimbali na kuzingatia maoni yao na serikali itaendelea kupokea maoni ya wadau  hata mara baada ya kusomwa kwake.
Pamoja na hayo Waziri huyo mwenye dhamana na sekta ya habari nchini  kupitishwa kwa Muswada huo kutasaidia kutoa suluhisho la kuwepo na changamoto katika sekta ya utangazaji ambayo kwa sasa inaonekana kupoteza mulekeo.

Aidha,Waziri Nnauye alisema kuwa serikali inataka kuipeleka  tansia  ya habari mbali  na kupitia Muswada huo utasaidia kufanikisha hilo kwani umeeleza kuwa mwandishi anahitajika kuwa na digrii na hii ni kwalengo la kuweka heshima ya taaluma kama ilivyokwa taaluma nyingine mfano sheria.
Halikadhalika Waziri huyo alizungumzia kuwepo na changamoto  katika Sheria ya Utangazaji kwani imekuwa haionyeshi  Mtangazaji anaporusha kipindi hewani kilicho kinyume na maadili ni adhabu gani apewe.

“Tungependa sheria ijayo iweze kumbana mwandishi pale anapokosa maadili na kumchukulia hatua kama ilivyo kwa tansia nyingine kama uhandisi na sheria kufikia hatua kufutiwa utoaji wa huduma hiyo”,alisisitiza Mhe.Nnauye.

Akizungumza  kuhusu changamoto ya upatikanaji  wa taarifa kutoka kwa wasemaji wa taasisi za Serikali Waziri Nape alisema tayari ametoa agizo kwa watendaji kuwashirikisha wasemaji katika vikao vya maamuzi ili waweze kuwa na taarifa za pamoja na kuwapa nafasi ya kusema ikiwa na sehemu ya kazi yao.

Hata hivyo Mheshimiwa Waziri ameliahidi Shirika la Utangazaji nchi kulisaidia kutatua changamoto zinazolikabili ikiwemo uhaba wa vifaa,pamoja na kuboresha maslai ya watumishi wake.Pia ameeleza  Bodi mpya ya TBC 1 iliyoundwa  imepitia  mkataba wa TBC 1 na STARTIMES  kwa lengo la kutaka kuiboreshea mazingira shirika hilo na tayari imekwisha maliza kazi na kuwasilisha mapendekezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...