Na Eleuteri Mangi na Beatrice Lyimo, MAELEZO, Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amewataka wadau wa habari na wananchi kwa ujumla kutoa maoni juu ya Muswada wa Sheria ya Huduma ya Habari wa mwaka 2016 uliosomwa kwa mara ya kwanza Bungeni leo mjini Dodoma.
 
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhairishwa Bunge, Waziri Nape amesema kuwa muswada huo unalengo la kuboresha tasnia ya habari ili kuweza kurahisha utendaji kazi wa wanahabari na kuifanya tasnia hiyo kuheshimika nchini.
 
“Ombi langu kwa wadau wa tasnia hii wausome vizuri muswada huo na  kujitokeza kwa wingi na kutoa maoni yao ili tuwe na sheria itakayoleta magezuzi na kukuza tasnia ya habari” amesema Waziri Nape.
 
Waziri Nape amewataka wadau wa habari kuendelea kusoma muswada huo ili kuweza kupata mapendekezo ya namna ya kuifanya sheria hiyo kuwa bora kwa manufaa ya maendeleo ya taifa.Aidha, Waziri Nape amewaahidi wadau wa habari kukutana nao mara kwa mara wakati wa kutoa maoni na mapendekezo yao yatakayosaidia kuboresha mazingira ya wanahabari nchini ili waweze kufanya kazi yao ipasavyo wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kuhabarisha umma.
 

Vile vile, Waziri Nape amewapongeza waandishi wa habari kwa kushiriki vema katika kuhabarish umma kuhusu mkutano wa Bunge uliohitimishwa leo na kuahidi kuendelea kushirikiana nao wakati wote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...