Kushoto ni Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi akimkabidhi Mwenge Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Geofrey Mwambe tayari kwa ajili ya kumulika Miradi 18 katika Wilaya hiyo.
Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi Rehema S. Madenge.
 Timiza wajibu wako kata Mnyoro wa Rushwa
Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi akisoma salamu za shukrani mara baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma katika Kijiji cha Lusilile

Na Mathias Canal, Singida
KATIBU tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi leo ameupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi Rehema S. Madenge ambao utakimbizwa Mkoani Singida kwa siku saba katika Halmashauri saba ambapo utaanzia Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.

Dkt Lutambi amekabidhiwa Mwenge huo pamoja na wakimbiza Mwenge Kitaifa katika eneo la Kijiji cha Lusilile Kata ya Kintinku Wilaya ya Manyoni ukiwa umewaka na kuahidi kuukabidhi kwa katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora pasina mashaka utakapomaliza muda wake Mkoani Singida.

Lutambi alisema kuwa mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani humo utalitia jumla ya miradi 61 inayohusu sekta ya ufugaji, Mazingira, Maji, Afya, Elimu, Barabara, Utawala Bora, Kilimo, Ushirika, Biashara, Ardhi na Programu za mapambano dhidi ya Dawa za kulevya, Malaria Rushwa na Ukimwi.

Alisema kuwa jumla ya Miradi 33 itazinduliwa, 13 itawekwa jiwe la msingi minne itawekwa jiwe la msingi na mingine mitano itatembelewa ambapo miradi yote hiyo itakayopitiwa itakuwa na thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 14.

Mbio za Mwenge wa uhuru kwa Mwaka 2016 zimebeba kauli mbiu ya "Vijana ni nguvu kazi ya Taifa, Washirikishwe na kuwezeshwa" ambapo hata hivyo kila Halamashauri nchini zimeelekezwa kutenga asilimia 5% ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya vijana na asilimia 5% nyingine kwa ajili ya kina mama.

Katika kumaliza mizizi wa Rushwa, Dawa za kulevya, ukimwi na Malaria Mwenge wa Uhuru umejikita zaidi katika kauli mbiu ya "Timiza wajibu wako kata Mnyororo wa Rushwa" kwenye mapambano dhidi ya Rushwa, Kauli mbiu ya "Tujenge jamii, Maisha na Utu wetu bila dawa za kulevya" kwenye Mapambano dhidi ya Dawa za kulevya, Kauli mbiu ya "Tanzania bila maambukizi mapya, Unyanyapaa na Vifo vitokanavyo na UKIMWI inawezekana" kwenye Mapambano dhidi ya Ukimwi na Mapambano dhidi ya Malaria, chini ya kauli mbiu ya " Wekeza katika maisha ya baadae, Tokomeza Malaria".

Kwa upande wake katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi Rehema S. Madenge wakati akikabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoani Singida alisema kuwa Mwenge wa Uhuru umekimbizwa katika Wilaya zote saba za Mkoa huo ambapo jumla ya Miradi 47 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 12.

Bi Madenge amewapongeza wananchi wote kwa ushirikiano na juhudi kubwa walizofanya katika kuianzisha, kuiendeleza na kuikamilisha Miradi yote.

Pia alisema kuwa katika Wilaya zote walizozuru wakimbiza Mwenge wamepata taarifa za utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Mwaka 2015 na kuelezea namna inavyoendelea kutekelezwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Geofrey Mwambe wakati akikabidhiwa Mwenge wa uhuru na katibu Tawala wa Mkoa wa Singida amesema kuwa Mwenge huo unataraji Kutembelea Miradi 18 ambapo hii leo utatembelea miradi 7 na hapo kesho utatembelea Miradi 11.

Miongoni mwa Mirafi itakayofunguliwa ni pamoja na uzinduzi wa Programu  ya Ufuatiliaji na kuteketeza mbu, Kufungua Mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu nane ya vyoo na ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa, Ufunguzi wa daraja la Makutupora, Kuzindua Klabu ya  wapinga Rushwa, Kuzindua Mradi wa Ujenzi wa kituo cha Maarifa ya kupambana na UKIMWI, Kuzindua Mradi wa Vijana wa kufyatua matofali, na Kuzindua Klabu ya Kupambana na Dawa za Kulevya.

Kwa mujibu wa ratiba za mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka huu, unakimbizwa katika Halmashauri na Manispaa zipatazo 179 na kilele cha mbio hizo ni Octoba 14 mwaka huu katika Mkoa wa Simiyu.

Mwenge wa Uhuru unaashiria Nuru na Mwanga, Uliwashwa rasmi kwa mara ya awali juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro Disemba 9, 1961.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...