Watu kadhaa wamepoteza maisha na nyumba nyingi  Mkoani Kagera zimebomoka baada ya tetemeko la Ardhi lenye nguvu ya 5.7 kipimo cha Ritcher kupita kwenye mikoa hiyo ya Kanda ya Ziwa.
Taarifa zinadai Mji wa Kamachumu Mkoani Kagera ndio umeathiriwa Vibaya na tetemeko hilo, ambapo nyumba nyingi zimebomolewa.

Kiasi cha watu 10 wamepoteza maisha na mamia kujeruhiwa kwa  mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Augustine Ollomi.

Nyumba Moja wapo ambayo imeathirika na Tetemeko hilo lililotokea Muda mfupi uliopita Mjini Bukoba.

Nyumba ikionekana kupata nyufa baada ya tetemeko la Ardhi kuutikisa Mji wa Bukoba hivi Punde

Milango ya Geti katika nyumba hiyo ikionekana kuanguka chini baada ya kukumbwa na dhoruba ya tetemeko la Ardhi, lililotikisa Mji wa Bukoba.
Baadhi ya Nyumba za Wananchi wa Mji wa Bukoba Zikiwa katika hali Mbaya baada ya Tetemeko la Ardhi Kupita.


Gari ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mjini 

Bukoba likiwa katika harakati za Uokoaji. 
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Poleni.
    Ila tuache kutumia mafundi tutumie wahandisi kudizaini nyumba zetu.

    Hatujui lini tetemeko jingine litatokea, linda nyumba yako na uhai wako kwa kutumia wataalam ambao kodi yako ndo inawasomesha.

    ReplyDelete
  2. Poleni sana wana Kagera. Ili ni janga la taifa na tupo pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu. Tunamuomba Mungu awapunzishe kwa amani wale waliotutangulia na kuwapa haueni na matumaini wote waliopatwa na janga hili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...