Afisa  Masoko na Elimu kwa Umma wa  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Hawa Duguza akitoa maelekezo kwa mwanacha  njisi ya kujaza  fom leo katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
 Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Yusuph Kitainda akisisitiza jambo kwa wangeni alietembelea kambi ya (NHIF) leo katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa (NHIF) wakiwa katika kambi ya hoyo leo katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya wa NHIF umeaandaa mkakati wa kutatua kero za wanachama wake kwa kuwafata katika maeneo yao ya kazi.

Zoezi hilo limeanzia katika Wilaya ya Ilala ambapo Mfuko umeweka kambi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa muda wa siku tatu ili kuweza kutatua kero na kufanya marekebisho madogo madogo ya kadi za NHIF kama kwa watu waliopotelewa na kadi, kubadilisha au kuongeza mwenza, kutoa barua za utambulisho wa Polisi kama kadi imepotea.

Pamoja na kutatua kero hizo Mfuko pia unatoa elimu kuhusu bima ya afya hiyo na kuwahimiza wananchi kutembelea banda lao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...