Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umefanya maboresho ya bei za huduma za afya zinazotolewa na mfuko huo ikiwemo huduma ya upasuaji na ada ya kumuona daktari.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam leo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga amesema kuwa kutokana na maboresho hayo baadhi ya huduma zimepanda bei, nyengine zimeshushwa bei na nyengine hazijabadilishwa bei ili kumuwezesha mtumiaji wa huduma hizo kuzimudu gharama na kupata huduma zilizo bora.

Aidha Konga amesema kuwa mabadiliko ya bei na mabadiliko ya aina za huduma hazitaathiri ubora wa huduma wala uwezo wa mwanachama kuhudhuria vituo vya matibabu pindi atakapohitaji huduma kwa kuwa huduma za afya zinazingatia taratibu za tiba.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Masuala ya Kitaalamu, Dkt. Aifena Mramba amesema kuwa mabadiliko makubwa ya upandaji wa bei yamefanyika kati ya yale yaliyopita na ya sasa ikiwemo upasuaji wa moyo na vipimo vya moyo umeongezeka bei pamoja na upasuaji wa uzazi na kufunga mirija ya uzazi nao umeongezeka kutokana na tathimini zilizofanyika katika soko na watumiaji wa huduma.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga akizungumza na waandishi wa habari juu ya maboresho ya bei za huduma za afya zinazotolewa na mfuko huo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurungenzi wa Uendeshaji wa NHIF, Christopher Mapunda.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Masuala ya Kitaalamu (NHIF), Dkt. Aifena Mramba akifafanua jambo kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bernard Konga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...