Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) itaanza kutoa Vitambulisho vipya vya Taifa vyenye saini kwa wananchi wote waliokamilisha taratibu za usajili na utambuzi na kuchukuliwa alama za kibaiolojia (Alama za vidole, Picha, Saini ya Kielektroniki).

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bw. Andrew Massawe; utekelezaji wa zoezi hilo utaanza rasmi Jumanne tarehe 14 Septemba 2016 katika ofisi zote za NIDA zikiwemo ofisi za Wilaya zilizoanza usajili Tanzania Zanzibar na mikoa ya Dar-es-salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, na Ruvuma) pamoja na waheshimiwa Wabunge Dodoma.

Waombaji wote ambao Vitambulisho vyao viko tayari watatumiwa ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) katika simu zao za kiganjani (mkononi) kufahamishwa kufika katika vituo vya Usajili kuchukua Vitambulisho vyao.

Kuhusu wananchi ambao tayari wana Vitambulisho visivyo na saini; Bw. Massawe amesema…. “ Mamlaka inakusudia kubadilisha vitambulisho vyote vya zamani visivyo na saini, ila kwa sasa vitambulisho vya zamani vitaendelea kutumika sambamba na vipya wakati taratibu za kuendelea kuvibadilisha zikiendelea” alisisitiza.
Amesema kutokana na uwepo wa njia nyingi na salama za kusoma taarifa za mwombaji zilizomo ndani ya kifaa maalumu kilichofichwa kwenye kadi ya mtumiaji (chip); ndiyo maana vitambulisho vya zamani vitaendelea kutumika katika huduma mbalimbali zinazohitaji kumtambua mtumiaji kabla ya kupata huduma.

Akizungumzia wananchi ambao hawakuwahi kusajiliwa, Bw. Massawe amesisitiza kwamba wananchi wote ambao hawakuwahi kusajiliwa na wana umri wa miaka 18 na kuendelea; kwa mikoa ambayo tayari kuna ofisi za usajili, kuendelea kujitokeza kwa wingi kusajiliwa ili kupata Vitambulisho vya Taifa kwani zoezi la usajili ni endelevu.
“Kwa wale wananchi ambao walisajiliwa kupitia Daftari la Mpiga kura NEC; NIDA iko mbioni kuanza kutoa nambari za utambulisho wakati tukiendelea kukamilisha taratibu za usajili ili kupata utambulisho kamili na kuanza kunufaika na matumizi mapana ya Utambulisho wa Taifa wakati taratibu za uzalishaji wa Vitambulisho zikiendelea”.


Wananchi wanakumbushwa kutunza vizuri Vitambulisho vyao ili kuepuka gharama kwani kitambulisho cha Taifa kwa mara ya kwanza kitatolewa bure na iwapo kitapotea, ili kupata kingine lazima mtumiaji akilipie.

Kwa sasa vitambulisho vya Taifa vimeanza kutumika katika baadhi ya huduma nchini hususani kwenye mabenki kwa ajili ya kufungua akaunti na kuthibitisha taarifa za mtu kabla ya kupatiwa huduma.  Taratibu za kupanua wigo wa matumizi ya Vitambulisho kielektroniki kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali zinaendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. kuhusu vitambulisho, hizo namba nadhani ni nyingi mno na hazieleweki kirahisi. nimeona mifano ya nchi nyingine ambazo kunakuwa na namba za mwaka wa kuzaliwa + namba nne au tano tu. mf kwenye kitamulisho kilichowekwa 19870805-14131 tu na huwa inatosha kutoa utambulisho na pia mtu kukumbuka hiyo namba.

    ReplyDelete
  2. tuambiwe, hiyo signature ni ya nani hapo? mtoaji au mwenye kadi?

    ReplyDelete
  3. Na vp kwa upande wa watu wanaoishi nje ya tanzania watapata vp?

    ReplyDelete
  4. Vitambulisho vya zamani kwenye mabenki mengin nchini hukataliwa kwa vile havina sahihi ya mwenye kitambulisho. Nadhani ni kwa vile Mabank hawana "card readers" kwa ajili ya kusoma taarifa zilizopo katika kitambulisho. NIDA wangeanza na wenye vitambulisho vya zamani kubadilishia wateja ili wananchi waepukane na usumbufu.

    ReplyDelete
  5. Nunga mkono maoni yaliyotelewa hapo juu. Ila nipo na dukuduku..Hii expire date ni ya nini!

    Ina maana huo muda ukifika (Expire date), mmiliki ana cease kuwa Raia!
    Naomba some reasonable explanation.

    ReplyDelete
  6. Mdau wa #3, hata huko ulimwennguni vina tarehe ya mwisho, kutokana Na kubadilika sura,kumbuka sura ya miaka 20 sio ya 30.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...