Mkuu wa Kitengo cha Miamala wa benki ya NMB, Michael Mungure akizungumza na waandishi wa habari juu kufanyika malipo na usajili wa makampuni pamoja na ulipaji wa ada kwa Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA) leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Meneja wa Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA), Bosco Gabi
BENKI  ya NMB  imesema kuwa wananchi wanaweza kupata huduma kwa Wakala wa  Usajili wa Makampuni (BRELA) kwa kutumia benki  kutokana na kuwa imeenea nchi nzima.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Miamala wa benki hiyo, Michael Mungure amesema kuwa malipo ya usajili wa makampuni kwa sasa yatafanyika kupitia benki ya NMB katika matawi yote ikiwa ni pamoja na katika mifumo ya simu ya NMB Mobile ikiwa ni kurahisisha wananchi kuondokana na gharama ya kusafiri kupata huduma hiyo.

 Amesema makubaliano  hayo na NMB na BRELA ni fursa ya watu kusajili makampuni bila usumbufu kutokana na benki kuwa karibu na wananchi.

‘’Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA kuwa  makampuni kuanza  kulipa ada za usajili kupitia mifumo NMB ‘’Alisema Mkuu wa Kitengo cha Mihamala Michael Mungure .

Mungure amisema kuwa huduma hiyo imeshakamilika ikiwemo mifumo ya taasisi hiyo itakayo wawezesha makampuni kuweza kulipa kutumia benki hiyo popote alipo katika matawi au kwa njia ya simu.

Nae Kaimu Meneja wa Wakala wa Usajili wa Makampuni BRELA, Bosco Gadi amesema kuwa benki ya NMB ni benki ya kwanza inayodumisha ushirikiano na taasisi  katika utoaji huduma za usajili na ulipiaji ada kwa makampuni .

Gadi amesema kuwa taasisi yake inajishughulisha na usajili wa viwanda na majina mbalimbali ya Biashara  ikiwemo kusajili makampuni kupitia tozo mbalimbali za usajili wa makampuni .
Amesema kuwa wanaendelea kuelimisha wananchi katika utoaji wa huduma hiyo na wataanzia kutoa elimu mkoani Mwanza.

‘’Hii nifursa nzuri ya kurasimisha biashara na kupunguza gharama za kutafuta huduma za BRELA ‘’Amesema Gadi .

Gadi amsema kuwa walipofikia na NMB  itawezesha wafanyabiashara kurasimisha biashara zao nakuiwezesha serikali kuweza kupata mapato na kukuza uchumi wa taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...