Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefakiwa kukamata watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi hatari ambao wamekuwa wakishiriki matukio mbalimbali ya uhalifu kwa kutumia silaha.
Watu hao wanaodaiwa kuwa majambazi walipatikana na bunduki 23 za aina tofauti tofauti, Risasi 835, kifaa cha kuzuia risasi kuingia mwilini tatu (Burret Proof), Sare za Polisi, Pingu 48 pamoja na Radio 12 za mawasiliano.
Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya kanda maalum, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Sirro amesema kuwa majambazi hao walikuwa na mtandao mkubwa ikiwa ni kununua silaha nje ya nchi kwa ajili ya kufanyia uhalifu katika maeneo mbalimbali.
Kamanda Sirro amesema baada ya tukio hilo timu ya polisi ya upelelezi iliweka mtego na kufanikiwa kukamata majambazi watatu maeneo ya Mbagala, Keko na Kawe.
Kamanda Sirro amesema katika mahojiano walikiri kufanya tukio katika benki ya Habib African maeneo ya Kariakoo 2014 na Stanbic 2014.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro
akionyesha kifaa cha kuangalia wakati wakifanya uhalifu majambazi kwa
waandishishi wa habari ikiwa ni sehemu ya vifaa vilivyokuwa vikitumika
na majambazi sugu leo katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo
jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro
akionyesha bunduki kwa
waandishi wa habari ikiwa ni sehemu yabunduki zilivyokuwa zikitumika
na majambazi sugu leo katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo
jijini Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro
akizungumza na waandishi habari juu ya operesheni walioifanya na
kukamata majambazi watatu katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo
jijini Dar es Salaam.
Kusoma zaidi bofya HAPA.
Kusoma zaidi bofya HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...