Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea picha ya mfano wa Daraja jipya la Salenda litakojengwa kuanzia maeneo ya Hospitali ya Agha Khan na kupita baharini  hadi eneo la Coco beach jijini Dar es Salaam kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Song Geum-Young aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilomita 7 na kati ya hizo kilomita 1.4 zitapita baharini na ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwezi Juni mwakani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha  Balozi wa Urusi hapa nchini Yuri Popov aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa  nchini Song Geum-Young mara baada ya kupokea picha hiyo ya mfano wa Daraja jipya la Salenda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...