Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 01 Septemba, 2016 amemuapisha Bw. Doto M. James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Bw. Doto M. James aliteuliwa kushika wadhifa huo jana tarehe 31 Agosti, 2016 na amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Servacius Likwelile ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Doto M. James alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera).
Hafla ya kuapishwa kwa Bw. Doto M. James imehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
Aidha, Bw. Doto M. James amekula kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma, zoezi ambalo limeongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda.

 Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es salaam
01 Septemba, 2016 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Doto James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Fedha na Mipango Doto James mara baada ya kuapishwa.PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. MKUU WA NCHI HII PICHA YA LEO NDIYO SAWA, NYUMA YENU HAKUNA WATU WNGINE, HII SASA NAONA MNAKUWA WA KIMATAIFA.
    DR, JAMESY

    ReplyDelete
  2. Ajira za watoto wa wakulima na wafanyakazi zimesahulika!!! Miezi miwili iliyosemwa imeshatimia!!! Bring back our employment

    ReplyDelete
  3. Kweli kabisa. Picha ya leo safi sana. Keep it up.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...