Na Abel Daud-Globu ya Jamii Kigoma

Mkuu wa Mkoa wa kigoma Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga amezipongeza idara ya kukusanya mapato TRA,kituo cha manyovu pamoja na Jeshi la polisi Wilaya ya kipolisi manyovu kwa juhudi kubwa za ukusanyaji wa mapato na ulinzi wa eneo hilo.

Maganga ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya siku tatu aliyoifanya katika Wilaya ya buhigwe ya kukagua miradi mbalimbali pamoja na kusikiliza changamoto zinazoikabili Wilaya hiyo.

Pamoja na pongezi hizo,Maganga ameonyesha kukerwa na baadhi ya tabia za wafanyakazi wa idara hizo kutuhumiwa kujihusisha na upokeaji rushwa na kuwataka kuacha mara moja tabia hyo kwani inatia aibu kubwa taifa letu na kuwaomba wawe waaminifu.

Akisoma taarifa fupi kwa Mkuu wa Mkoa,Afisa mfawidhi wa TRA kituo cha Manyovu ndugu Yusuph Haji ameeleza jinsi idara hiyo ilivyofanikiwa kupanda kwa mapato,ambapo kwa mwaka 2015-2016 kituo hicho kilipangiwa kukusanya shilingi 32,998,122 milion na kufanikiwa kukusanya shilingi 48,135,704 milion,ameongeza kuwa kwa mwaka 2016-2017 kituo kimepangiwa kukusnya shilingi 63,750,366 ambapo mpka sasa kituo kimefanikiwa kukusanya shilingi 17,092,536 sawa na asilimia 27 ya malengo ya mwaka huu.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe  Kanali Elisha Gaguti amemshukuru Mkuu wa mkoa wa Kigoma na kumuahidi kusimamia maagizo yote aliyoyatoa na kuwataka watendaji wote wa halmashauri hiyo kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na kuwaomba kuendana na kasi hii ya serikali ya awamu ya tano.

 Mkuu wa Mkoa wa kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga  akiwasha moto katika tanuru la matofali, tayari kwa uzinduzi wa benki ya matofali ktk kijiji cha Kibwigwa,mkoani Kigoma.

 Mkuu wa Mkoa wa kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga 
(wa tatu kushoto) akitoka kukagua ujenzi wa nyumba za walimu ktk shule ya sec Nyamirambo


 Mkuu wa Mkoa wa kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga  
pia alikagua utendaji kazi wa ofisi ya TRA kituo cha Manyovu 

 Mkuu wa Mkoa wa kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga akikagua eneo la benki ya matofali kijijini hapo
 Mkuu wa Mkoa wa kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga akipata maelezo ya mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa ktk shule ya sec Nyamirambi kata ya Kajani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...