TIMU ya Serengeti Boys leo imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Congo Brazaville katika mchezo wa kufuzu kuingia fainali za mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 nchini Madagascar  uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo ulioanza kwa kasi na kila upande kushambuliana kwa zamu zilianza kuzaa matunda kwa timu ya Serengeti Boys kuandika goli la kwanza dakika ya 38 liliolofungwa na Yohana Mkomola na dakika ya 42 akafanikiwa kuongeza goli la pili kwa Serengeti Boys.

Mpaka inafikia mapumziko Serengeti Boys walikuwa mbele kwa goli 2-0 lakini dakika ya 73, Langa-Lesse Percy anaiandikia Congo Brazzaville goli la kwanza kwa mkwaju wa penati baada mchezaji kuangushwa ndani ya eneo la hatari.
Issa Makamba anaipatia Serengeti Boys goli la tatu akitumia nafasi nzuri aliyoipata lakini halikudumu sana katika dakika ya 90 Poboumela Chardon akaipatia Congo Brazzaville goli la pili kwa kutumia uzembe wa goli kipa Kelvin Kayego aliyeingia kuchukia nafasi ya Ramadhan Kabwili aliyeumia wakati akiokoa penati.
Mpaka mpira unamalizika Serengeti Boys wametoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 3-2.
Kila timu iliweza kufanga mabadiliko na kwa upande wa Serengeti Boys walimtoaYohana Mkomola na kuingia Issa Makamba, Ibrahim Ali na kuingia Muhsin Makame na kwa Congo Brazaville alitoka Mboungou Prestige na kuingia Mountou Edoward, Mantourari Aldo na kuingia Makoina Beni na Kiba Konde Rodrique na kuingia Bopoumela Chardon.
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Vijana "Serengeti Boys", Yohana Oscar Mkomola akikimbilia upande walipo mashabiki mara baada ya kuipatia timu yake Goli, katika Mchezo wao dhidi ya Congo Brazaville wa kuwania kufuzu kucheza katika Mashindano ya Kombe la Afrika la Vijana chini ya Miaka 17, yatakayofanyika Nchini Madagascer mwakani. Serengeti Boys imeibuka na ushishi mwembamba wa bao 3-2, hivyo watajipanga kwa mchezo wa marudiano utakaochezwa juma lijalo. Magoli ya Serengeti Boys yamefungwa na Yohana Oscar dakika ya 38 na 42 na Issa Abdi Makamba dakika ya 70, huku magoli ya Congo Brazaville yakifungwa na Langa-Lesse Percy kwa mkwaju wa penani na dakika ya 90 Poboumela Chardon. 

Shambulizi la hatari langoni mwa Timu ya Serengeti Boys.Mchezaji wa timu ya Serengeti Boys,Yohana Oscar Mkomola akitoka mbio maara baada ya kuachia mkwaju mkali kwa golikipa wa timu ya Congo Brazaville,na kutinga wavuni,likiwa ni goli la pili mnamo dakika ya 42 kipindi cha kwanza.
Mabeki wa Timu ya Congo Brazaville wakiusindikiza kwa macho mpira uliopigwa vizuri kabisa na Mchezaji wa Serengeti Boys, Issa Abdi Makamba na kuipatia timu yake bao la tatu, katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza katika Mashindano ya Kombe la Afrika la Vijana chini ya Miaka 17, yatakayofanyika Nchini Madagascer mwakani.
Beki wa Timu ya Taifa ya vijana ya Congo Brazaville, Moundza Prince akiwa ameruka juu kuondosha hatari iliyokuwa imeelekeswa langoni kwake, katika mchezo dhidi ya Serengeti Boys uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...