Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO.

Serikali imesema kuwa inashirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuhakikisha kuwa madereva wanaoendesha magari aina ya malori ambao wametekwa nyara jana na waasi wa kikundi cha Maimai katika eneo la Namoyo jimbo la Kivu kusini katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanapatikana wakiwa salama.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuwakoa watanzania waliotekwa nyara.

“Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Kongo inaendelea kufanya kila jitihada kuhakikisha madereva hao wanaachiwa huru haraka iwezekanavyo na kurudishwa nchini wakiwa salama”

“ Waasi hao wa Maimai wametoa masaa 24 hadi kufikia leo wawe wamelipwa kiasi cha Dola 4,000 kwa kila dereva ili waweze kuwaachia huru na kutishia kuwadhuru endapo hawatapata fedha hizo, hivyo basi Serikali imeendelea kuwa na mazungumzo na Serikali ya Kongo ili kupata ufumbuzi wa suala hili” alisema Kasiga.

Aliongeza kuwa malori yaliyotekwa nyara ni 12 kati ya hayo nane ni mali ya mfanyabiashara wa kitanzania Bw. Azim Dewji na mengine ni mali za wafanyabiashara kutoka nchini Kenya.Aidha, Serikali imewataka watanzania kufahamu hali ya usalama wa nchi wanazokwenda ili kujikinga na matatizo mbalimbali yanayoweza kuwapata wakiwa katika nchi hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...