Kikundi cha wahitimu wa elimu ya juu SUJA ECO-ENERGY wakiwa na mfano wa hundi ya dola 3000 ambayo wamekabidhiwa baada ya kubuni wazo la kijasiriamali la mradi wa kutengeneza nishati kupitia kinyesi cha ng’ombe.
 Kikundi cha wahitimu wa elimu ya juu cha RECHA wakikabidhiwa mfano wa hundi ya dola 3000 kutoka kwa Mkurugenzi wa Teknolojia na Operesheni  wa Benki ya Posta Tanzania Bw.Jema Msuya . Benki ya Posta Tanzania ni moja ya waliodhamini mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wahitimu wa elimu ya juu.
Kikundi cha wahitimu wa elimu ya juu cha GBL Bucket Toilet Co. wakiwa katika picha ya pamoja na mwakilishi kutoka mfuko wa ubunifu wa maendeleo kwa binadamu (HDIF)Bw. David McGinty baada ya kujishindia dola 3000.Wahitimu hao wameshinda pesa izo baada ya kubuni mradi wa kutengeneza choo ambacho kinatumia ndoo ya plastic
Na Daudi Manongi,MAELEZO


Na Daudi Manongi- MAELEZO ,Dar es Salaam

Serikali kupitia Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi limesema kuwa litaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini ili kutatua changamoto ya ajira kwa vijana.

Hayo yamesemwa juzi Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Vijana katika Ofisi ya Waziri Mkuu, James Kajugusi wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wahitimu wa elimu ya juu nchini.

“Uwezeshaji wananchi kiuchumi ni dhana pana inayohitaji ushirikiano wa karibu kati ya serikali na sekta binafsi pamoja na wadau wa maendeleo na katika kuchochea juhudi za uwezeshaji wananchi kiuchumi” alisemaBw.Kajugusi

Akizungumzia kuhusu changamoto zinazowakabili vijana nchini, Kajugusi alisema kuwa changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana imechochewa na mabadiliko ya kisera na kiuchumi yanayosimamiwa kwa dhati na serikali katika kupeleka mbele zaidi taifa letu katika nyanja za kijamii na kiuchumi.

Awali akizungumza na vijana 22 waliohitimu mafunzo hayo aliwataka vijana hao kuongeza ari ya kufanya kazi na kushiriki fursa mbalimbali zinazojitokeza zenye lengo la kujikwamua kiuchumi.

“Vijana mtumie vema fursa mbalimbali za uwezeshaji mnazozipata kwa kuboresha zaidi uelewa wenu na hali zenu za maisha” Alisema Kajugusi

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi, Bi Anna Mtaita amesema kuwa Baraza hilo litaendelea kuthamini nchini na kwa kulitambua hilo maana wameamua kushirikiana na taasisi ya maendeleo ya Cambridge katika kuratibu na kutoa mafunzo hayo.

Mtaita aliongeza kuwa mbali na programu hiyo, Baraza hilo pia linaratibu programu ya majaribio kwa vijana walio katika mazingira magumu katika kuwapatia mafunzo, malezi, na kuwaunganisha na mitaji.

Kwa mujibu wa Mtaita alisema mpaka kufikia sasa Baraza hilo limewawezesha vijana 500 nchini katika upataji wa mafunzo, malezi na mitaji. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...