UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema hakuna mazungumzo, majadiliano wala mijadala inayostahili kufanyika kati ya Serikali ya CCM na Chadema na kuiomba Serikali ya Rais Dk John Magufuli iendelee na mikakati yake ya kisera ili kuimarisha maendeleo ya kiuchumi.
Pia umoja huo umeeleza kuwa dunia inajua, ulimwengu unaaelewa na Chadema wanafahamu kuwa Tanzania hakuna mgogoro wa kisasa zaidi ya serikali kupigania mabadiliko, nchi kuwa ya viwanda na kutokomeza maadui umasikini, ujinga na maradhi.
Msimamo huo umetolewa jana na Kaimu Katibu Mluu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ukumbi wa White House Makao Makuu ya CCM Mkoani hapa.
Shaka alisema UVCCM ilijua, ilielewa na kutambua mapema Chadema na viongozi wake walikuwa wakifanya maigizo katika siasa, hawakuwa na ubavu wala jeuri ya kuandamana kwa madai aliyoyaita ni ya kipuuzi ambayo hayana msingi kwa mustakabali wa nchi na maendeleo yake.
Alisema viongozi na wafuasi wa Chadema walishindwa kuandamana Septemba Mosi, hawataweza na wala hawatajaribu kufanya hivyo Oktoba Mosi kwa sababu wanachotaka kukifanya ni utoto wa kisiasa baada ya kushindwa kubuni mkakati wa kukiendesha chama chao ili kiaminike na kukubalika.
"Tunazo habari wabunge wa Chadema wamechachamaa na kumbana Mbowe kwa hoja wakitaka kurudi bungeni ili kushiriki vikao kwa kuwa hawaeleweki kwa wapiga kura wao majimboni lakini pia wanakabaliwa na 'waya mkali', hawaoni kwa nini wasishiriki vikao vya Bunge huku baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho wakiwa na utajiri na wengine wafanyabiashara,"alisema Shaka.
"Cha ajabu hata na wale wazee tuliokuwa tukiwaheshimu bila soni wanashiriki kuudanganya ulimwengu wakitoa madai ati kuna mgogoro wa kisiasa unaohitaji suluhu, yafanyike mazungumzo na majadiliano,"alisema Shaka.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...