Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (mb) amesisitiza kuwa dhamira ya Serikali kuhamia Dodoma ipo palepale ndani ya kipindi cha miaka minne hatua kwa hatua.

Akizungumza na waandishi wa habari Septemba 2, 2016 wakati wa ziara yake eneo la Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim yaliyopo Mlimwa Dodoma, Waziri Mhagama alisema “Watanzania wawe na amani, dhamira yetu iko vizuri na kama Mhe. Rais alivyosema na tunawahakikishia kwamba ndani ya kipindi hicho sisi tumeshajipanga kuhamamia mkoani Dodoma hatua kwa hatua”.

Waziri Mhagama alieleza kuwa shughuli za maendeleo hazitosimama kwa kuzingatia mipango iliyopo na bajeti ya Serikali, “Niwatoe wasiwasi kwamba mipango yote ya maendeleo haitosimama na shughuli zote za maendeleo hazitozuiwa na ujio wa Serikali mkoani Dodoma zitafanyika kama zilivyopangwa na tutaendelea kuyafanya hayo kwa kuzingatia Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 Ibara ya 151 tumesema tunahamia Dodoma na tutafanya hivyo”.Alisisitiza Mhagama

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana ameahidi kutekeleza usimamizi wa maagizo ya Waziri ili kukamilisha ujenzi wa barabara kwa wakati “kwa upande wa mkoa kazi iliyobaki ni kuhakikisha kuwa ujenzi wa barabara unakamilika na tutakutana na Wakala wa Barabara (TANROADS), Mamlaka ya Ustawishaji Mji (CDA) na Manispaa ili kuona shughuli hii tunaifanyeje kwa kutekeleza maagizo hayo ikiwa ni sehemu ya majukumu ya mkoa.”

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana alimshukuru Waziri Mhagama kwa kutembelea maeneo ya makazi mapya ya Mhe. Waziri Mkuu na Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,”Namshukuru Mhe. Waziri Mhagama, Manaibu Waziri na Ofisi yote ya Waziri Mkuu kwa ziara hii na kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu.” 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akifuatilia maelezo ya ramani ya Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim kutoka kwa Wataalam wa maswala ya Ujenzi kulia kwake ni Mhandisi Joseph Muhamba na wa kwanza kushoto ni Bw. Keffa Chana wakati wa Ziara yake katika makazi hayo Septemba 2, 2016 Mlimwa Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagam (katikati) akipata maelezo ya eneo la Makazi Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim kutoka kwa Mtaalam wa Masuala ya Ujenzi Bw. Keffa Chana alipofanya ziara ya kukagua makazi haya Septemba 02, 2016 Mlimwa Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...