Mwanafunzi aliyeongoza masomo yote Rahma Mdea akipokea cheti cha
kuhitimu darasa la saba na zawadi yake wakati wa mahafali ya shule
ya Southern Highlands Mafinga
Mwanafunzi
aliyeongoza masomo yote Rahma Mdeka akipokea cheti cha kuhitimu darasa
la saba na zawadi yake wakati wa mahafali ya shule ya Southern
Highlands Mafinga
Mkurugenzi wa shule za Southern Highlands Mafinga ,Mary Mungai kulia akitambulisha watumishi wa shule hiyo. …………………………………. Na MatukiodaimaBlog UONGOZI wa shule ya Southern Highlands Mafinga wilayani Mufindi umewataka wazazi wa wanafunzi zaidi ya 50 waliofanya mtihani wa Taifa wa darasa la saba katika shule hiyo kuanza kuwa na uhakika wa watoto wao kufaulu mtihani huo . Huku ukiahidi kutoa kuchangia sehemu ya ada kwa wanafunzi watakajiunga na shule ya sekondari ya Southern Highlands Mafinga kama sehemu ya ahsante kwa ushirikiano ambao wazazi wamekuwa wakitoa kwa shule hizo. Mkurugenzi mtendaji wa Southern Highlands Mafinga Mary Mungai aliyasema haya jana wakati wa mahafali ya darasa la saba shuleni hapo . “Shule hii ilianza mwaka 1994 kama Day Care na Pre-School. Mwaka 1997 ikakuwa na kuanza shule ya msingi-Primary School mwaka 2001 shule ilitoa wanafunzi wa kwanzawa darasa la saba wanafunzi walikuwa 17,wote walifauru vizuri na wote walichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza Katika matokeo ya mitihani ya darasa la 7 ya mwaka 2001 Southern Highlands School ilishika nafasi ya kwanza kitaifa katika mitihani yasomo la kiingereza ” Alisema kuwa matokeo mazuri ya wanafunzi wote kufaulu mitihani ya kitaifa ya darasa la saba yamekuwa ni kawaida kwa shule hiyo na kuwa toka kuanzishwa kwake haijapa pata kufelisha hata mwanafunzi mmoja . Hivyo kuwataka wazazi kutokuwa na hofu juu ya wanafunzi hao waliofanya mtihani mwaka huu kwani waanze kujiandaa kwa kuwapeleka sekondari. Wakati huo huo mkurugenzi wa familia ya Lucy Chawe inayoishi nchini marekani na Tanzania imepongeza jitihada za shule hiyo na kuahidi kuendelea kuiunga mkono serikali kwa kuhamasisha masomo ya Sayansi na Hisabati kwa wanafunzi Mkurugenzi wa The Chawe Foundation Award , Kitove Mungai alisema kuwa kila mwaka wamekuwa wakitoa zawadi kwa wanafunzi wa Awali hadi darasala saba ambao wamekuwa wakifanya vizuri masomo ya Hisabati na sayansi . Aliwataja wanafunzi ambao wamepewa zawadi hiyo kwa mwaka huu kuwa ni Brayan Mgomapayo, Rahma Mdeka na Ayub Toss ambao walifanya vizuri katika hesabu . Wakati katika sayansi wanafunzi waliopewa zawadi ni Nimrod Nyakunga , Rahma Mdeka na Erick Mwanjelwa . |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...