KIWANDA Cha Saruji Cha Simba (Simba Cement) cha Tanga, kimeipa shule ya Sekondari ya Ilboru Secondary School ya Arusha mifuko 400 ya saruji yenye thamani zaidi ya milioni 4.8 kwa ujenzi wa vymba vya madarasa.

Akizungumza wakati wa halfa fupi ya makabidhiano leo, Mkuu wa Idara ya Rasilimaliwatu kiwanda cha Saruji cha Simba Cement, Diana Malambugi, alisema msaada huo umetolewa ili kupunguza changamoto za vyumba vya madarasa kwa shule hiyo.

Alisema msaada huo utapunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na kutoa wito kutumika kama ilivyokusudiwa na kuiagiza kamati ya shule kuhakikisha mifuko hiyo inatumika ipasavyo.

‘Mifuko hii ya saruji itapunguza changamoto inayoikabili shule yako ikiwemo vyumba vya madarasa na ujenzi wa nyumba za walimu, sera yetu moja wapo ni hii ya elimu” alisema Malambugi

Alimtaka mwalimu huyo na kamati yake ya shule kuitunza mifuko hiyo ya saruji na kumhakikishia kuisaidia pale ambapo kutakuwa na uhitaji na kuwataka wadau wengine wa elimu kusaidia sekta ya elimu zikiwemo kuondosha changamoto za uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa.

Kwa upande wake, mwalimu mkuu wa shule ya Ilboru sekondari school , Julias Shulla, alikishukuru kiwanda hicho na kusema kuwa msaada huo utatumika kama ilivyoombwa.

Alisema shule yake inakabiliana na changamoto nyingi zikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja uhaba wa vifaa vya maabara hivyo kuwataka wadau wa elimu kuisaidia.

‘Tunakishukuru kiwanda cha saruji cha simba kwa moyo wao waliounyesha kwetu, kwa fadhila hii tunawaahidi kuwa tutaitumia saruji kama tulivyoiomba” alisema Shulla

Alisema mifuko hiyo itapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ambazo shule yake inakabiliana nazo na kusema kuwa msaada huo ni faraja kwao na wanafunzi wa shule yake.
Mkuu wa Idara ya Rasilimawatu kiwanda cha Sauji cha Simba Cement cha Tanga, Diana Malambugi, akimkabidhi mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya milioni 4.8 kwa mwalimu mkuu shule ya Sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla ikiwa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa.nyuma kulia ni Mkuu wa fedha Pieter Jaggar na kushoto ni Emmanuel Jonas mhasibu.
Mhasibu wa kiwanda cha Saruji cha Simba Cement, Emmanuel Jonas, akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari ya Iboru ya Arusha, Julias Shulla mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 4.8 kwa ajili ya ujenzi wa vymba vya madarasa, nyuma ni mkuu wa fedha, Pieter Jaggar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...