Timu ya Azam FC "Wanalambalamba" na Wekungu wa Msimbazi Simba SC wanakutata kukipiga jioni ya leo katika mtanange wa kuwania nafasi ya kuongoza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. 

Timu hizo zinakutana leo ikiwa zote zinatiana kabali kwa kuwa na pointi na wastani wa magoli yao pia, baada ya mechi nne za awali huku kila moja ikiwa imeshinda mechi tatu na kutoa sare moja moja, hivyo ayakayefanikiwa kupata ushindi kwenye mtanange huo, ndie ataushikilia usukani wa Ligi kuu kwa sasa.

Timu ya Globu ya Jamii iko tayari tayari kukuletea matukio mbalimbali katika picha ya Mchezo huo, hivyo usikae mbali na libeneke lako hili pendwa kupata taswira mwanana kabisa za Mchezo huo.
Kikosi cha Azam Fc.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...