SIMU.TV: Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, ametoa wito kwa viongozi nchini kuwatumikia wananchi wao na kuacha kutumia madaraka kujinufaisha wenyewe;https://youtu.be/OSvATdFGIQA

SIMU.TV: Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako, ameitaka tume ya vyuo vikuu nchini TCU kuvifuatilia na kufahamu sifa za vyuo nchini na sio kugeuka kuwa madalali wa vyuo;https://youtu.be/c0nGuZfHo58

SIMU.TV: Wakazi wa baadhi ya vijiji wilayani Newala mkoani Mtwara, wameelezea furaha yao ya kumalizika kwa kero ya maji baada ya kukamilika kwa mradi wa maji safi na salama;https://youtu.be/Tvm2n58KyuQ

SIMU.TV: Waziri wa viwanda na biashara Charles Mwijage, amewataka wanawake wajasiriamali kuwa na uthubutu mkubwa wa kufanya biashara kubwa kubwa;https://youtu.be/oKmk1YFTog4

SIMU.TV: Kaimu kamishina wa uchambuzi wa masuala ya fedha wa wizara ya fedha Augustini Ollao, amesema mashindano ya fedha na mikopo nchini yanasaidia kuimarisha sekta ya uchumi; https://youtu.be/UXO-DrUEoAw

SIMU.TV: Maonyesho ya 98 ya shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidigo yanatarajia kuanza kesho mkoani Mbeya ili kutoa fursa kwa wenye wajasiriamali wadogo kujifunza;https://youtu.be/WVH3vZiYLIk

SIMU.TV: Tiketi za kielekitroniki kwa ajili ya mchezo wa Yanga na Simba tayari zimeanza kuuzwa ili kuondoa usumbufu kwa wateja ambao wengi ni wageni wa mfumo huu;https://youtu.be/_FuLusb4tko
SIMU.TV: Timu zinazoshiriki ligi daraja la nne mkoa wa kisoka wa Kinondoni zimetakiwa kuonyesha kandanda maridadi ili kuweza kuwavutia mashabiki wao;https://youtu.be/gcoYh5aVcj4

SIMU.TV: Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umeanzisha mashindano ya michezo kwa wananchi wanaozunguka mgodi huo ili kuweza kuwa na mahusiano mazuri na kupunguza migogoro na wananchi; https://youtu.be/TlzPUnKflRY

SIMU.TV: Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Mauritius anashikiliwa na jeshi la polisi nchini humo kwa tuhuma za kukutwa na kete kadhaa za madawa ya kulevya;https://youtu.be/YPWuEealrMY

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...