Meneja Mauzo Kitaifa wa Tanga Simenti, Leslie Massawe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati wa kuitambulisha bidhaa mpya ya Mkombozi-Simenti ya Mwendo Kasi jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja wa mambo ya nje na mawasiliano wa Tanga Simenti, Mtanga Noor
 Meneja Mauzo Kitaifa wa Tanga Siment, Leslie  Massawe(Wapili kutoka Kulia) akiwa na wafanyakazi wa Tanga Simenti wakionesha mfuko wa Simenti wa Kilo 50 wakati wa uzinduzi na kuitambulisha bidhaa hiyo mpya ya Mkombozi-Simenti ya Mwendo Kasi jijini Dar es Salaam leo. 

TANGA Cement Public Limited Company (TCPLC) wazalishaji wa simenti hapa nchini wamezindua bidhaa bora ya simenti inayoitwa, MKOMBOZI.
 “Bidhaa hii mpya ya Tanga Cement ni hatua nyingine ya kuwa karibu na Watanzania kwa kubuni na kuwaletea aina nyingine ya simenti, ambayo mbali na kuwa ni ya bei ya kuridhisha kwa Mtanzania wa kawaida bado inawahakikishia ubora dhabiti unaoendana na teknolojia ya kiwango cha juu katika utengenezaji wa simenti”.

Ameyasema hayo wakati wa kuitambulisha bidhaa hiyo mpya ya Mkombozi-Simenti ya Mwendo Kasi, Meneja Mauzo Kitaifa wa Tanga Simenti, Leslie jijini Dar es Salaam leo.

Amesema kuwa mahitaji ya wananchi ni makubwa kukabiliana na ongezeko la miradi ya miundombinu na wakati huo huo mahitaji ya simenti bora katika ujenzi miundombinu na nyumba za makazi katika maeneo ya mijini na hasa vijijini ambapo utaalamu katika ujenzi.

Bidhaa mpya ya simenti ya MKOMBOZI – ‘simenti ya Mwendokasi' inaletwa kwa Watanzania ili kuharakisha maendeleo ya makazi bora na shughuli nyingine za ujenzi kama jina linavyojieleza.

MKOMBOZI, simenti ya daraja la nguvu kwa kiwango cha 32.5 N, ni simenti ambayo   bei yake ni ya kuridhisha ambapo mtu yeyote anayehitaji simenti kwa ujenzi wa aina yoyote anaweza kununua. 

Mkombozi imekuja kuwapatia watanzania kile wanachohitaji katika ujenzi wa miundombinu pamoja na makazi hii ni simenti kwa matumizi yote, simenti kwa aina zote za ujenzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...