Kampuni ya TanzaniteOne ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, imejipanga kuhakikisha kuwa inaendelea kuunga mkono michezo mbalimbali ili kuhakikisha wanamichezo wanapiga hatua.

Ofisa mahusiano wa kampuni hiyo Halfan Hayesh  alisema japokuwa TanzaniteOne imedhamini michezo mingi hadi sasa, itaendelea kujitolea mara kwa mara kuwasaidia wanamichezo.

Alisema hivi karibuni walimdhamini mwanamichezo wa mbio za magari na pia wakazifadhili timu nne za soka za mkoa wa Manyara, kwa kuzipatia vifaa vya michezo ikiwemo suti na sare za michezo, mipira, na sare za waamuzi.

“Tunawaahidi wapenzi wa michezo kuwa tutaendelea kuwadhamini wanamichezo kwani hivi karibuni tulidhamini gari moja kwenye mbio za magari na kuwakilishwa na dereva Shanbhai na msaidizi Mwangi,” alisema Hayesh.

Alisema pia walishadhamini michezo mingine ya burudani ikiwemo ya miss kanda ya kaskazini, miss Arusha, Miss Manyara na Miss Mirerani na wataendelea na udhamini wa michezo tofauti ili kusaidia maeneo yote.

Alisema anatambua kupitia michezo kuna vipaji vingi vitagunduliwa hivyo kampuni hiyo itaendelea kuthamini suala hilo kwani michezo ni ajira, afya, upendeo, furaha, burudani na kujenga mshikamano na jamii inayowazunguka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...