Mkuu wa kitengo cha fedha wa benki ya DTB, Joseph Mabusi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa utiaji wa saini wa mkataba wa udhamini wa ligi kuu Vodacom wenye thamani ya Milioni 250 kwa msimu wa mwaka 2016/17,na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali pamoja na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini Rais Jamali Malinzi.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF Jamal Malinzi akitia saini mkataba wa udhamini wa ligi kuu Vodacom wenye thamani ya Milioni 250 akiwa sambamba na Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya DTB Joseph Mabusi ikishuhudiwa na waandishi wa wa habari na viongozi wengine wa Bodi ya ligi pamoja na wawakilishi kutoka katika timu za ligi kuu.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF Jamal Malinzi wakikabidhiana mkataba wa udhamini wa ligi kuu Vodacom na Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa DTB Joseph Musiba wenye thamani ya Milioni 250.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Nchini TFF limeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Milioni 250 na Benki ya Diamond Trust kwa ajili ya udhamini wa ligii kuu ya Vodacom.

Mkataba huo wa msimu wa mwaka 2016/17, DTB wanaungana na wadhamini wengine ikiwa ni lengo la kuziwezesha timu hususani kwenye maendeleo ya soka nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini mkataba huo, Rais wa TFF Jamali Malinzi amesema kuwa amezitaka taasisi nyingine kuiga mfano huo kwani kwa kufanya hivyo kutawawezesha kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi kuu.

Malinzi amesema kuwa, kuanzia sasa huduma zote za tiketi za kieletroniki zitakuwa chini ya benki ya Diamond Trust kwa msimu wa 2016/2017.

Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya DTB  Joseph Mabusi amesema kuwa udhamini huu utasaidia zaidi kukuza soka na pia wanajivunia kuwa sehemu ya ligi kuu na wanaamini udhamini huu utazidisha ari ya kuwahudumia watanzania wote.

Mabusi amesema, mbali na kuidhamini ligi kuu Vodacom pia wanadhamini timu ya ligi daraja la tatu Agathon iliyopo Mbagala na nia wadhamini wa michuano ha Afrika Mashariki na Kati CECAFA Kagame Cup mwaka 2015.

Mkataba huo utakuwa chachu ya maendeleo ya soka kwa nchi pamoja na kuzifanya timu kujituma zaidi uwanjani pia unatarajiwa kuwa endelevu na kila mwaka kutakuwa na mabadiliko mbalimbali kwenye mkataba huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...