Kufuatia hali inayoukabili
mkoa wa Kagera kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo mnamo
septemba 10 mwaka huu na kusababisha maafa makubwa kwa baadhi ya Wananchi na
hata kuchukua uhai wa watu 17 Mkoani humo
Shirika la Maendeleo ya Petrol
Tanzania (TPDC) limeungana na jitihada za Serikali katika kusadia waathirika wa
tetemeko Mkoani humo kwa kutoa vifaa vya
ujenzi ikiwa ni pamoja na saruji na mabati vyenye thamani ya shilingi millioni
20 kwa ajili ya kusaidia ujenzi kwa walioguswa na maafa hayo.
Baada ya kukabidhi vifaa
hivyo kwa Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu, Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji TPDC Mhandisi, Kapuulya Musomba amesema kuwa wametoa vifaa hivyo
vyenye thamani ya shilingi millioni 20 kwa ajili ya kuwasadia waathirika wa
tetemeko hilo.
Pia Mhandisi Musomba
amesema kuwa misaada waliotoa sio mwisho badala yake watahakikisha wanaendelea
kuwafuatilia kampuni washirika wanaofanya kazi na TPDC nchini, huku akiongeza
kuwa tayari wameshawaandikia barua ya kuwaomba kuchangia na kushiriki katika
kusaidia Wanakagera.
Kaimu
Mkurugenzi wa TPDC Mhandisi, Kapuulya Musomba akipeana mikono na Mkuu wa
Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu mara baada ya kukabidhi msaada
wa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni ishirini (20,000,000) kwa
waathirika wa tetemeko Mkoani Kagera.
Mjumbe
wa Bodi ya TPDC Balozi Ben Moses akikabidhi nyaraka zenye orodha ya vifaa vya
ujenzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu vilivyo
kabidhiwa na TPDC.
Zoezi
la kukabidhi misaada iliyotolewa na TPDC kwa waathirika watetemeko Mkoani
Kagera likiendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...